Chigaitan mapinduzi vijijini
JOHN BILLY TENDWA, Msajili wa zamani wa vyama vya siasa, Aliyepata Mafanikio makubwa katika kuimarisha, kudumisha na kuendeleza ustawi wa Demokrasia nchini Tanzania amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili leo.
John Billy Tendwa alikuwa Msajili wa vyama kwa miaka (2001-2013) akichukua nafasi ya Jaji George Bakari Liundi mwanzilishi wa vyama vya siasa 1992 mpaka 2001 na Tendwa kuja kuvistawisha.
Chigaitan mapinduzi vijijini mara ya mwisho amekutana na John Billy Tendwa 2019 kanisa la Mt. Joseph kwenye misa ya kwanza. John ni miongoni mwa wakatoriki safi nchini Tanzania na mfano mkubwa kwa vijana wa leo.
Nikisema Mkatoriki Safi maana yake alipenda sala maisha yake yote can you imagine umri wa John Tendwa hakosi ibada za Kanisa tena uwapo Kanisani Sauti yake inasikika ikiimba sala za kumtukuza Mungu huyu alikuwa binadamu wa kipekee katika Sala.
John Billy Tendwa alifanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Msajili wa vyama hatua inayomfanya kuwa baba wa demokrasia nchini Tanzania.
John Billy Tendwa aliwezesha kupelekwa Bungeni miswada mbalimbali ya Sheria na kufanikisha kuwa sheria (The Political Parties Act No.7/ 2009 na "The Political Parties Code of Conduct" na pia alishiriki kwenye utungwaji wa _"Election Expenses Act 2010" sheria zilizoleta mapinduzi makubwa ya uwanja sawa wa demokrasia nchini Tanzania.
Mtakubalina na Chigaitan mapinduzi vijijini kuwa John Billy Tendwa kipindi chake ndiyo Sauti za wapinzani tuliona matunda yake ya thamani ya upinzani na vyama vya siasa.
Tulijua ufisadi serikalini, Tuliona kuanguka kwa mawaziri wakuu, tuliona kuvunjwa kwa baraza kwa kashifa za ubadhilifu wa fedha za umma,
Tuliona jinsi fedha za Umma zinasafirishwa nje ya nchi, Tuliona jinsi kampuni "Fake" zinaanzishwa kuchota fedha za umma kwa maslahi binafsi.
Leo tunaposhuhudia safari ya mwisho ya John Tenda serikali ina mifumo imara na bora ya matumizi na Ufuatiliaji wa fedha ya umma HAKUNA ufisadi tena serikalini nchini Tanzania.
Leo tunaposhuhudia Umauti wa John Billy Tendwa Bunge lina mbunge mmoja tu aliyechaguliwa na wapiga kura kwa demokrasia ya taifa letu.
Leo tunaposhuhudia kifo cha John Billy Tendwa taifa likiwa na giza la upinzani wenyewe wakikanyaga demokrasia Mbowe akitaka Uwenyekiti wa Chadema
Ikumbukwe Mbowe akiwa mwenyekiti wa CHADEMA John Tendwa ndiyo alikuwa anachukua nafasi ya msajili wa vyama vya siasa mwaka 2001.
Pumzika kwa amani baba wa Demokrasia John Billy Tendwa.


