Wadau wa Mazingira Wakutana Kujadili Namna ya Kutokomeza Majanga Kwenye Makazi duni

GEORGE MARATO TV
0


Tatizo la uchafuzi wa mazingira ikiwemo utiririshaji wa maji taka kutoka kwenye makazi yaliyoko kwenye maeneo ya miinuko Jijini mwanza kwenda kwenye ziwa victoria limepungua baada ya baadhi ya wananchi waishio kwenye maeneo hayo kunufaika na mradi wa ujenzi wa vyoo bora.

Mradi wa ujenzi wa vyoo kwenye maeneo ya Miinuko umetekelezwa na Taasisi ya kujenga uwezo na ubunifu wa Jamii nchini CCI Kupitia muungano wa vikundi vya kijamii vilivyoko kwenye makazi duni Jijini Mwanza.


Miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na ujenzi wa vyoo bora ni pamoja na Mtaa wa Mabatini Kusini ambapo baadhi ya wakazi walionufaika na ujenzi wa vyoo wamelishukuru Taasisi ya CCI kwa kuwaondolea changamoto ya Ukosefu wa Vyoo uliokuwa unawakabili.

Wakazi hao Rhobi Samwel na Jackline George wamesema kuwa kabla ya kujengewa vyoo hivyo walikuwa wanatumia vyoo visivyokuwa na ubora na hivyo kuchangia uchafuzi wa mazingira ikiwemo Mto mirongo unaotiririsha maji yake kwenye ziwa victoria.

Akizungumza wakati wa ziara ya Wanachama wa muungano wa vikundi vya kijamii kutoka baadhi ya Mataifa barani Afrika waliotembelea eneo la Mabatini Mwanza,Mkurugenzi wa CCI Dokta Timothy Ndezi amesema kuwa zaidi ya vyoo 50 vimejengwa kwenye maeneo mbalimbali ya Miinuko Jijini mwanza.


Dkt.Ndezi amesema kuwa maeneo mengi ambayo yalikuwa hayana vyoo bora watu walikuwa wanapata kipindupindu na magonjwa mbalimbali lakini baada ya kazi ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa Kushirikiana na Muungano wa Vikundi vya Kijamii Mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira.

‘’Ziwa Victoria lina mchango mkubwa katika Maisha ya watu, watu wasipokuwa na vyoo bora maana yake uchafuzi unakuwa mkubwa zaidi,kwa hiyo shirika letu limekuwa likifanya kazi na vikundi vya kijamii katika kutatua tatizo la vyoo kwenye maeneo ya milimani lakini vilevile tumekuwa tukitoa elimu kwa Jamii kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na upandaji wa miti kwenye maeneo mbalimbali’’alisema Dkt.Ndezi

Mkuu wa kitengo cha habari na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mwanza MWAUWASA Vivian Temu kuwa Katika kukabiliana na majanga hasa mabadiliko ya tabia nchi kwenye maeneo ya miinuko,Mwauwasa imekuja na Mfumo rahisi wa uondoaji wa Maji taka ambao umewezesha wakazi waliopo kwenye miinuko kuunganisha vyoo vyao kwenye Mfumo wa maji taka.

‘’Hii imesaidia Kupunguza Uchafuzi wa Mazingira kwenye baadhi ya Maeneo ya Milimani hasusani wakati wa Mvua nyingi ambayo yanapata majanga kipindi cha mvua nyingi ikiwa ni pamoja na changamoto ya kuwa na vyoo vya kisasa vya kuondoa maji taka kutoka kwenye maeneo yao lakini pia kuzuia uchafuzi wa mazingira tulikuja na mfumo rahisi wa uondoaji kwenye maeneo ya miinuko’’alisema Vivian

Wanachama wa muungano wa vikundi vya kijamii kutoka Tanzania pamoja na mataifa ya Kenya,Zimbabwe,Malawi,Ghana na Afrika Kusini wako Jijini Mwanza kubadilishana ujuzi wa namna ya kuzuia ama kupunguza maafa kwenye makazi duni.













 

 

 

 


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top