Mwenyekiti wa CCM Simiyu afanikisha kupatikana milioni 33.2 za maendeleo ya kanisa

GEORGE MARATO TV
0

 

Ni mwana Mama Shemsa Mohamed,apewa hati ya pongezi

Kanisa KKKT lamshukuru jinsi alivyojitoa kufanikisha harambee hiyo

Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Bi Shemsa Mohamed ameungana na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika harambee ya kuchangia maendeleo ya kanisa hilo.

Katika harambee hiyo imelega kuchangia ujenzi wa hosteli na uzio wa kanisani,ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu na usalama wa kanisa wa hilo.

Akishiriki katika tukio hilo, Mwenyekiti Shemsa Mohamed, pamoja na wadau wengine, wamefanikiwa kuchangia kiasi milioni 15,000,000 kati ya TSh 33,200,000 zilizokusanywa kwenye harambee hiyo.

 Mchango wake ulipongezwa kwa kuwa ni mfano wa kujitoa kwa dhati kusaidia taasisi za dini na jamii kwa huku viongozi wa kanisa wakintaja kama kiongozi wa mfano.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo,mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed amesisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano kati ya taasisi za dini na Serikali katika kuleta maendeleo ya jamii.

 Amebainisha kuwa CCM, kama chama tawala, kinaunga mkono juhudi za kijamii zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi na kudumisha amani na mshikamano nchini.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa mfano jinsi anavyojitoa kuchangia huduma za jamii zikiwemo za kidini bila ubaguzi hivyo kutaka viongozi wote kuiga mfano huo.

Waumini wa KKKT pamoja na viongozi wa kanisa walitoa shukrani zao za dhati kwa Mwenyekiti Shemsa Mohamed kwa mchango wake mkubwa na kwa kuthamini kazi ya Mungu kupitia kanisa.

 Harambee hiyo inatarajiwa kusaidia kukamilisha miradi ya ujenzi wa hosteli na uzio, hatua ambayo itaongeza thamani na huduma za kijamii kupitia kanisa hilo.

Kwa kumalizia, Mwenyekiti Shemsa aliwahimiza wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu kuendelea kushirikiana katika miradi ya maendeleo, huku akitoa wito wa kudumisha amani, mshikamano, na maadili mema.

_"Mshikamano wetu ndiyo msingi wa maendeleo. Tukidumisha upendo na kushirikiana, kila jambo linawezekana,"_ *alisema Mwenyekiti Shemsa Mohamed*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top