Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali yabainisha Mikakati ya Kurejesha hadhi ya Madini ya Tanzanite


-Waziri Mavunde azindua mnada wa ndani Mirerani leo.

- Minada ya ndani na nje ya nchi kutumika kutangaza madini ya vito.

-Madini yote yatakayokosa wanunuzi kurejeshwa kwa wahusika

-Wadau waonesha nia ya kujenga Mji wa Kimadini Mirerani


Mirerani

MANYARA: Waziri wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde amesema Serikali imejidhatiti kurudisha hadhi ya Tanzanite kwa kufanya minada ndani na nje ya nchi ili kuyaongezea thamani na wafanyabiashara waweze kunufaika na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 14, 2024 Mirerani mkoani Manyara wakati akizindua mnada wa madini ya vito ambao mara  ya mwisho ulifanyika mwaka 2017.

Mheshimiwa Mavunde amesema mojawapo ya maeneo yanayosaidia kuongeza mapato ni pamoja na kudhibiti biashara ya madini, kuzuia utoroshaji na kuifanya biashara hiyo kuwa katika mfumo sahihi, uwepo wa minada utachochea uongezaji thamani ya madini ya vito.

“Madini ya Vito  yananunuliwa kwa asilimia kubwa kwa ajili ya ‘luxury’ ni ufahari na  madini ya vito tunashindana na watu wengine ndio maana Serikali inaendelea kuchukua hatua, tunarudisha hadhi ya Tanzanite ili ikashindane vizuri duniani,”amesema Waziri  Mheshimiwa Mavunde na kuongeza, 

“Moja ya hatua ya kwanza ni urejeshaji wa minada ya ndani na ya kimataifa, ili tuyape thamani madini yetu, duniani kuna madini mengi ya vito, moja ya sifa kubwa ya madini ya vito ni uadimu, Tanzanite ina sifa hizo;  Ila sio madini pekee yake adimu,  kuna nchi nyingine zina madini adimu ambayo hayapatikani popote hivyo tunashindana kimataifa ni lazima tuchukue hatua kuhakikisha tunarudisha hadhi ya Tanzanite katika soko la kimataifa ili na bei iweze kuongezeka na wafanyabiashara wanufaike,”amesisitiza Waziri Mavunde

Amesema, katika vipengele (category)   vya  mawe duniani,  jiwe linaanzia kuwa Precious, semi-Precious halafu baadaye linakuwa jiwe la kawaida na kwamba wanachukua hatua za makusudi ili  Tanzanite lisiwe jiwe la kawaida.

“Tukiacha liwe la kawaida mtanunua kwa kilo kwa gharama ndogo sana na mtashusha hadhi ya Tanzanite, Serikali haipo tayari kuona hilo linatokea ndio maana tunayafanya haya kwa ajili ya kuhakikisha tunalinda hadhi na heshima ya jiwe letu hili.” Amesisitiza Mheshimiwa Mavunde.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde amewahakikishia wadau wa madini kuwa Serikali haitachukua  madini ya mtu baada ya mnada wa leo na kama kuna  madini yatabaki yatakabidhiwa kwa wahusika.

“Kumekuwepo na hisia na dhana baada ya mnada Serikali itachukua madini yaliyobaki kwa sababu katika mnada wa mwisho wa mwaka 2017 kuna madini yalibaki na wahusika hawakurejeshewa mpaka leo, nataka niwahakikishie Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kusimamia kuhakikisha katika biashara hii pia tuwajengee ‘confidence’ mtafanye biashara kwa uhuru na hakuna namna yoyote kuwa serikali itawaingilia na kuja kuyachukua madini yenu.

“Yale madini yaliyochukuliwa yapo,  yalibaki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tumeshayatoa na tutawakabidhi rasmi wahusika ili waendelee  na biashara yao ya madini, nataka niwatoe hofu na muwe na amani,”amesema Waziri Mavunde.

“Manyara tayari mna eneo ambalo tutajenga ‘Tanzanite Exchange Centre’ ambayo kwa sasa tumefanya mazungumzo na wadau tutajenga kitu kinaitwa ‘Tanzanite Smart City’ ambao utakuwa mji mkubwa wenye hoteli ndani yake, Helikopta ambazo zitatua humo humo, ukumbi mkubwa wa mikutano wahusika hivi sasa wapo Wizara ya fedha, likikamilika hili natamani siku moja mkutano mkubwa wa madini ufanyike Mirerani.”Amesema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ameongeza kuwa kupitia mnada huu uliozinduliwa leo, idadi ya wauzaji waliojisajili kwenye mfumo wa kielektroniki wa kuendesha minada ni 195 wakiwemo wafanyabiashara wadogo wa madini (brokers) 120, wafanyabiashara wakubwa wa madini (dealers) 59, waongeza thamani madini (lapidary) 7 na wachimbaji madini 9. Kiasi cha madini kilicholetwa kwenye mnada ni kilogramu 184.06 kinachokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 3.10. 

Wakati huohuo akizungumza kwenye uzinduzi wa mnada huo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Kilumbe Ng’enda amempongeza Waziri wa Madini kwa kuweka nguvu kubwa kwenye utafiti wa madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na kuwezesha wachimbaji kuchimba bila kupoteza mitaji ikiwa ni sehemu ya “Vision 2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri,” na kuongeza kuwa,

“Kamati itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara lengo likiwa ni kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini unakua na kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025”

Naye Mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka amepongeza jitihada za Serikali kwa kupania kuleta mapinduzi ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini, kuhakikisha dhahabu inanunuliwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hivyo kuendelea kuimarisha uchumi wa nchi.

“Ninashauri Serikali kuendelea kutilia mkazo wa biashara ya madini ya vito kuendelea kufanyika katika mji wa Mirerani wakati ujenzi wa Soko la Madini Mirerani ukiendelea” amesisitiza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara , Mheshimiwa Queen Sendiga ameongeza kuwa minada ya madini ya vito italeta manufaa makubwa kwa nchi ikiwa ni pamoja na kukuza kipato kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, serikali kupata mapato, kuimarisha ubora wa madini ya vito na kuongeza ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.










Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...