Rais Dk.Mwinyi azindua Bodi Mpya ya Bmf

GEORGE MARATO TV
0

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishauri Bodi mpya ya Wadhamini ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa kuhakikisha inaendelea kuwa chombo cha kuaminika na Watanzania kwenye kuimarisha sekta ya afya ndani na nje ya nchi kama ilivyo Dira ya Taasisi hiyo.

Rais Dk Mwinyi ameyasema hayo alipozindua Bodi Mpya ya BMF hafla iliofanyika  Ukumbi wa BMF Kawe, jijini Dar es Salaam.

Rais Dk. Mwinyi ambae ni Msarifu wa taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ameeleza kuwa ni vema kwa sifa za wajumbe wa taasisi hiyo  kuendelea kudumu ndani ya taasisi  ili kuwavutia washirika zaidi na kuhakikisha ukuaji endelevu wa  kuwahudumia  walengwa wa taasisi hiyo.

Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi  amefafanua kuwa   Mpango Mkakati wa Taasisi hiyo utakaodumu kuanzia Julai 2024 hadi Juni 2030  utategemea Bodi na Menejimenti katika kutekeleza  na kufikia malengo yaliowekwa na kusisitiza umuhimu wa kudumisha rekodi nzuri ya utawala Bora, Uongozi mahiri, Utendaji wa kazi  wa taasisi hiyo. 

Rais Dk.Mwinyi ambae pia ni Msarifu wa BMF  amempongeza Mwenyekiti wa  Bodi ya Wakurugenzi wa  "Imara Horizon Company", Balozi John Ulanga na  wajumbe wenzake kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo la "Mkapa Health Plaza" kwa kipindi cha miezi 12 tangu alipoweka jiwe la Msingi Julai 2023. 

Akizungumza katika Hafla hiyo, Mwenyekiti Mpya wa BFM Balozi, Liberata Mulamula  ameahidi kwa bodi hiyo kufanya kazi kwa karibu na Serikali zote mbili za SMT na SMZ katika kufikia malengo  na Dira ya taasisi Hiyo

Rais Dk. Mwinyi  alikabidhi  vyeti maalum vya Ushirikiano na  Shukrani kwa Wajumbe wa bodi   ya BMF  waliomaliza muda wao  pamoja  kukabidhi nyaraka muhimu kwa Bodi Mpya kwa ajili ya utekelezaji ikiwemo Ripoti   maalum ya Miaka mitano . 

Hafla hiyo ya uzinduzi wa Bodi mpya ya BMF pia ilihudhuriwa  na Mjane wa Hayati Benjamin Mkapa,  Mama Anna  Mkapa.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top