Chama cha mapinduzi mkoa wa Mara kimefanya kikao chake cha kawaida cha halmasha kuu ya mkoa kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kiasiasa ya kuwezesha kushinda na kushika dola.
Katika kikao hicho cha kawaida ambacho kimefanyika mjini Musoma chini ya mwenyekiti wake Patrick Chandi pamoja na mambo mengine kimefanya tathimini ya uchaguzi wa Serikali za mitaa ulifanyika mwisho mwa mwezi novemba mwaka 2024.
Pia kikao kimewashukuru wanachama na wananchi ambao wamekiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Katika kikao hicho wajumbe wameendelea kumshukuru mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dr Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoa wa Mara.
Kwa sababu hiyo, kikao hicho kimeendelea kuwaomba Watanzania kumuunga mkono Rais Samia na serikali inayoongozwa na CCM na kwamba CCM inaridhishwa na utekelezaji mkubwa wa ilani ya uchaguzi.


.jpg)

