MBUNGE WA VITI MAALUM MHE. SALOME MAKAMBA APIGA KURA KITUO CHA BUGWETO A JIMBO LA SHINYANGA MJINI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Salome Makamba, leo amepiga kura katika kituo cha Bugweto A, kilichopo Kata ya Ibadakuli, Jimbo la Shinyanga Mjini, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

Mhe. Makamba ameungana na wananchi wengine ikiwemo familia yake kushiriki katika zoezi hilo muhimu ambalo linaendelea kote nchini kwa lengo la kuchagua viongozi watakaowakilisha jamii kwenye ngazi za msingi

Uchaguzi wa serikali za mitaa ni miongoni mwa hatua muhimu za kidemokrasia, zinazotoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya maendeleo ya maeneo yao.

Kwa sasa, zoezi la upigaji kura linaendelea katika vituo mbalimbali, huku usimamizi wa uchaguzi ukifanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top