Mpango kuongoza makamanda na watanzania kuaga mwili wa mkuu wa majeshi mstaafu

GEORGE MARATO TV
0


MAKAMU wa Rais mh Dkt Philip Mpango kuongoza Maafisa Jenerali,  Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo na Askari wa JWTZ kuaga mwili wa mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri.

Mh Mpango atamwakilisha amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania mh Dkt SamiaSuluhu Hassan kuaga mwili huo leo novemba 01- 2024 katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam. 

Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika saa tatu asubhi kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea Butiama mkoani Mara kwa ajili ya shughuli ya mazishi.

Jenerali Musuguri alifariki dunia asubhi ya Oktoba 29 mwaka 2024 wakati akapatiwa matibabu hospitali ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza,enzi za uhai wake ameshika nafasi mbalimbali ndani ya jeshi hadi kuwa mkuu wa majeshi kuanzia mwaka 1980 hadi 1988 alipostaafu kwa heshima.

Jenerali Musuguri akiwa jeshini amekuuwa mkufunzi wa askari wakati wa ukoloni wa Mwingereza. Mwaka 1953 alimfundisha pia Idd Amin katika kambi ya mafunzo ya Kahawa Barracks nchini Kenya.

 Hivyo mwaka 1978 katika vita vya Kagera, Mwalimu aliingia vitani na Mwanafunzi wake na akamshinda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top