Naibu Rais mteule wa kenya Profesa Kithure Kindiki Kesho novemba mosi anatarajia kuapishwa kuwa Naibu Rais wa Kenya
Profesa Kindiki anachukua nafasi ya Rigathi Gachagua aliyeondolewa ofisini kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kuendeleza ukabila.
Kwa mujibu wa Tangazo lililotolewa usiku huu kwenye gazeti rasmi la serikali,Uapisho wa Profesa Kindiki utafanyika Kesho katika kituo cha kimataifa wa Kenyatta international convention Center(K.I.C.C) uliopo katika kaunti ya Nairobi kuanzia majira ya saa nne kamili za asubuhi.
Naye Kaimu Waziri wa usalama wa ndani na utawala wa kitaifa Musalia Mudavadi ametangaza siku ya Kesho kuwa sikukuu ya taifa ili kutoa fursa kwa wakenya kushiriki pamoja kufuatilia uapisho wa Naibu Rais mteule.
Profesa Kindiki anatarajia kuapishwa baada ya mahakamani kuu kuondoa zuio la kuapishwa lililokuwa limewekwa na mtangulizi wake Rigathi Gachagua.
Kindiki ambaye kwa sasa ni Waziri wa usalama wa ndani na utawala wa kitaifa anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka kaunti ya Tharaka-nithi iliyoko mashariki mwa uliokuwa Mkoa wa kati mwa kenya kushika wadhifa wa unaibu Rais.


