Naibu rais wa kenya aliyeondolewa ofisini Rigathi Gachagu agonga mwamba mahakamani

GEORGE MARATO TV
0




 Na Mwandishi Wetu ;Nairobi

Juhudi za Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa ofisini Rigathi Gachagua kusimamisha kuapishwa kwa Naibu rais mpya Profesa Kithure Kindiki zimegonga mwamba Leo alhamisi Oktoba 31.

Gachagua amepata pigo mara mbili,pigo la kwanza ni pale mahakama ya rufaa ilipokataa takwa lake la kusimamisha majaji watatu wa mahakama kuu walioteuliwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kusikiliza kesi ya kupinga kuondolewa ofisini huku pigo la pili likiwa ni mahakama kuu kuondoa zuio la kuapishwa kwa mrithi wake. 

Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama ya rufaa,Majaji watatu ambao Gachagua alikuwa akipinga kusikiliza kesi yake waliondoa agizo lililompa ahueni kwa wiki mbili tangu atimuliwe na Bunge la kitaifa na Bunge la Seneti pamoja na Rais William Ruto kumteua profesa Kithure Kindiki kuwa naibu rais.

Majaji wa mahakama ya rufaa Patrick kiage,Agrey Muchelule na George Odunga waliagiza kesi iliyowasilishwa na Gachagua isikilizwe novemba sita mwaka huu.

‘’Hatuwezi kuondoa amri ya kuzuia majaji wa mahakama kuu kwa wakati huu''walisema majaji watatu wa mahakama ya rufaa.

Gachagua alifika mahakama ya rufaa wiki iliyopita akitaka kubatilishwa kwa amri ya kutangazwa kwa jopo la majaji watatu wa mahakama kuu akidai uteuzi wao uliofanywa na naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ni kinyume na katiba.

Katika uamuzi wao,Majaji Anthony mrima,Eric Ogola na Freda Mugambi wamesema kuwa wadhifa wa naibu rais hauwezi kubaki wazi.


‘’Mahakama hii inabainisha kuwa ofisi ya naibu rais haiwezi kubaki wazi na hivyo mahakama itakuwa upande wa katiba ambayo inaeleza kuwa lazima wadhifa huo ujazwe’’majaji hao walisema.

Walibainisha kuwa kesi hiyo ina maslahi makubwa kwa umma na walijitolea kutoa uamuzi wa haraka kwa zaidi kesi 30  zilizokuwa mbele yao.

Kesi hizo ziliwasilishwa na makundi mbalimbali kuzuia Gachagua kuondolewa ofisini ambapo ziliunganishwa na kusikilizwa na hatimaye kutolewa maamuzi na majaji hao.

Bunge la seneti,Bunge la kitaifa na mwanasheria mkuu wa serikali walifika mbele ya majaji hao watatu wa mahakama kuu kutaka kuondolewa kwa agizo la kuzuia kuapishwa kwa Profesa Kithure Kindiki ambaye kwa sasa nu Waziri wa usalama wa ndani na utawala wa kitaifa.

‘’Maagizo ya muda ya kuzuia kuapishwa kwa Profesa Kindiki yaliyotolewa oktoba 18 mwaka huu na mahakama kuu ya Kerugoya yameondolewa’’,waliamua majaji hao na kuongeza kuwa Gachagua na walalamishi wengine wako huru kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Gachagua aliondolewa ofisini oktoba 17 mwaka huu huku Profesa Kindiki akiteuliwa na Rais William Ruto  na kuidhinishwa na Bunge la kitaifa siku iliyofuata kuwa naibu Rais wa kenya

Gachagua na walalamishi wengine hata hivyo walikimbilia mahakamani na kupata maagizo ya kuzuia kuapishwa kwa waziri huyo wa usalama wa ndani na utawala wa kitaifa kusubiri uamuzi wa kesi.

Gachagua alinainisha kuwa alinyimwa haki ya kusikilizwa kwa haki na Bunge la kitaifa pamoja ba Bunge la Seneti na kwamba ushiriki wa umma ulioendeshwa na Bunge la kitaifa haukufikia kiwango cha kikatiba.

Mwanasheria mkuu wa serikali Dorcas Oduor na Na Bunge yote mawili walipinga agizo hilo la kuzuia kuapishwa kwa Profesa Kindiki wakisema kuwa lilikuwa na athari kubwa ambazo zinaweza kuingiza nchi katika mzozo wa kikatiba.

Alhamisi Oktoba 31 mwaka huu,Majaji wa mahakama kuu walikubaliana nao kwamba katiba haitoi nafasi ya kuwepo pengo katika ofisi ya naibu rais.

Bila Gachagua kupata agizo kutoka mahakama ya rufaa,mchakato wa kumuapisha Profesa Kindiki unaweza kuendelea.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top