Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuwasaidia na kuwashauri watendaji wafanye kazi vizuri ili kuhakikisha anayoyaota Mhe. Rais kwa Watanzania yanatimia.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakala huo ulofanyika jijijni Mbeya.
“Mwenyekiti wa bodi mtakuwa na kazi kubwa ya kuwashauri watendaji hawa, niwaombe mtusaidie na kutushauri kwani wananchi wanataka barabara na bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka milioni 200 hadi kufika Tilioni 1.3”.
Hata hivyo ameitaka bodi hiyo kuwa wabunifu na kujipanga ili barabara zinazosimamiwa na TARURA zikamilike pia washirikiane na wataalam kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa hati fungani unakamilika na kuzinduliwa ili kuwasaidia wakandarasi wazawa.
Aidha, Waziri Mchengerwa ameipongeza TARURA kwa kazi kubwa wanayoifanya.




Comments
Post a Comment