Mch. Askofu Valentine Mbuki Katibu wa Wachungaji Klasta ya Misungwi amehitimisha kilele cha fainali mashindano ya Klasta Compassion CUP 23/24 ambapo AICT Mabuki wakibuka kidedea kwa upande wa wavulana kwa ushindi wa magoli 5 - 4 dhidi ya AICT Masasi,
Kwa upande wa wasichana AICT Kijima imeibuka na ushindi kwa kuichapa goli 1 sifuri timu ya KKKT Misungwi Huku kwa mpira wa PETE AICT Mabuki wakiichabanga magoli 35 kwa 32 timu ya AICT Kijima
Mashindano hayo ambayo yalishirikisha jumla ya timu 20,wavulana timu 10 na wasichana timu 10 na yamefanyika kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili hadi kufikia tamati yake katika uwanja wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Misasi.



Comments
Post a Comment