Na Shomari Binda-Musoma
SHEKH wa mkoa wa Mara Msabaha Kassim amewataka viongozi wa dini wakiwemo wa misikiti kutumia vizuri mafunzo yanayotolewa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata)
Kauli hiyo ameitoa leo julai 28/2024 alipokuwa akifunga mafunzo yaliyotolewa na Bakwata kwa viongozi hao yaliyohusu utunzaji na udhibiti wa takwimu na rasilimali
Amesema elimu na mafunzo ni jambo muhimu katika kupata utambuzi na kufanya uongozi kidigitali.
Msabaha amesema suala la elimu na kuongeza ujuzi limeelezwa kwenye Quran na anachofanya Mufti Shekh Abubakar Zuber ni jambo jema
Shekh huyo wa mkoa wa Mara amesema mtu anapaswa kuifuata elimu lakini Mufti ameamua kuwaletea hivyo ni vyema kwenda kutumia vizuri mafunzo waliyoyapata.
" Niwapongeze mlioshiriki mafunzo hayo na niwaoombe tukayafanyie kazi ili malengo yaliyokusudiwa yaweza kufanikiwa.
Walimu wa madrasa tuliopata mafunzo hayo tukayatumia kupata kakwimu za wanafunzi wetu na tutumie mafunzo kubadilika na kuacha mazoea",amesema
Mratibu wa mafunzo hayo mkoa wa Mara Juma Abdala mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi ya Mufti wa Tanzania na yana lengo la kuwafanya viongozi wa dini kufanya na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Asha Muhamed ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam ( JUWAKITA ) amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutekeleza majukumu yao kama viongozi.




Comments
Post a Comment