Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akiambatana na viongozi wengine wa Benki, amefanya ziara ya kikazi katika Kanda ya Magharibi ya Tanzania, ikijumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Simiyu, Shinyanga, na Mwanza.
Katika ziara hiyo ya wiki moja, Bi. Ruth Zaipuna amekutana na wafanyakazi wa Benki ya NMB, wateja, na wadau mbalimbali, akilenga kuimarisha uhusiano na kutoa mwongozo kuhusu utekelezaji wa mikakati ya Benki katika maeneo hayo.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Ruth Zaipuna amefanya vikao na viongozi wa baadhi ya mikoa hiyo yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi.
Aidha, ziara hiyo pia ilitoa fursa ya kusikiliza maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau na kudhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya Watanzania katika ngazi zote.
Ziara hii ni muendelezo wa juhudi zetu katika kuhakikisha huduma bora za kifedha zinawafikia Watanzania katika kila kona ya nchi.
#NMBKaribuYako











Comments
Post a Comment