Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania FEMATA ambae pia ni mwenyekiti wa kamati tendaji Mhe. John Wambura Bina, anataraji kuanza ziara maalum katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo ataambatana na mwenyekiti wa TAWOMA Bi. semeni John Malale, pamoja na viongozi waandamizi wa TAWOMA kanda ya nyanda za juu kusini.
Pamoja na Viongozi hao pia itaamabatana na viongoizi waandamizi wa kampuni ya bima kwa wachimbaji wa madini Tanzania (Cizass Insurance Brokers) na viongozi waandamizi wa kampuni ya vitambulisho vya Kisasa (Biometric Identification Cards) kwa wachimbaji wa madini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hii iliyotolewa na kurugenzi ta habari FEMATA makao makuu imesema akiwa katika awamu ya kwanza ya ziara yake Mhe. John Bina atatembelea mkoa wa Dodoma mnamo julai 30, mkoa wa Iringa Julai 31, Songwe August Mosi na Pili kisha atamalizia na Mkoa wa Mbeya.
Awamu ya pili ya Ziara hiyo itahusisha mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi na kisha Dar es salaam na Pwani.
Pia Agosti. 05 mwaka huu Bw Bina na atakua na kikao cha kamati tendaji ya FEMATA kitakachofanyika jijini Mbeya ambapo wajumbe wa kamati tendaji.
FEMATA chini ya uongozi wa John Bina umeonesha mabadiliko makubwa na kuifanya sekta ya madini kukua kila kukicha pamoja na kuongezeka kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Serikali.




Comments
Post a Comment