![]() |
Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo anatarajiwa kufanya ziara kwenye Kata ya Bukima yenye lengo la kufufua ari ya kuchangia miradi ya maendeleo.
Ziara hiyo itafanyika baada ya kumalizika kwa ziara na mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakaokuwa Bukima jumatano julai 31
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge imesema baada ya mkesha huo wa Mwenge Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo atafanya ziara maalum kwenye Kata ya Bukima yenye malengo ya kufufua ari ya wananchi kujitolea kuchangia miradi yao ya maendeleo.
Taarifa hiyo imesema ipo miradi iliyokwama zaidi ya miaka 5 Kata ya Bukima, ikiwemo kukosa maabara hata mmoja kwenye sekondari ya Kata huku vifaa vilivyochangwa na mbunge vikiwa stoo.
Mradi mwingine uliokwama ni wodi ya mama mtoto kwenyez ahanati ya Bukima ikiwa inajengwa kwa zaidi ya miaka mitano ambapo mbunge wa jimbo alichangia saruji ya ujenzi.
Katika Kijiji cha Butata
ujenzi wa zahanati umesimama kwa zaidi ya miaka mitano (5) ambapo pia mbunge wa jimbo alichangia saruji ya ujenzi wake.
baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru mbunge wa jimbo atatembelea Kata ya Bukima kwa malengo yafuatayo
kuendelea kuwashawishi wananchi na viongozi wao kukubali kuchangia miradi yao ya maendeleo
Kushawishi wananchi kuchangia nguvukazi kwenye ujenzi wa sekondari mpya inayojengwa Kijijini Butata serikali imetoa fedha nyingi kwenye mradi huu,wananchi kushiriki kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Kutumia fursa zilizopo za kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka Halmashauri yetu na kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi",imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kuchangia miradi ya maendeleo.

Comments
Post a Comment