Rais Ameniteua Kuwa Daraja Kati ya Dini na Serikali- Katambi

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amefanya Kikao Kazi na Viongozi wa Dini nchini huku akiwaeleza Viongozi hao kuwa ameteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa daraja Kati ya Viongozi wa Dini na Serikali ambapo amewaambia milango iko wazi kwa viongozi hao kuongea na kushauriana na serikali ikiwemo utoaji wa maoni mbalimbali kwa serikali lengo ikiwa kudumisha tunu ya Amani na kuhakikisha kuwepo kwa Utulivu nchini.

Amezungumza hayo leo,jijini Dar es Salaam katika kikao kilichohudhuriwa  pia na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi na Msajili wa Jumuiya,Emmanuel Kihampa ambapo Viongozi wa Dini takribani 45 wakiwa wamehudhuria Mkutano huo.



*“Nimebeba dhamana hii kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan na Nchi yetu kuwa kiungo muhimu cha mahusiano, Usalama, amani na maendeleo au Daraja la kuvusha mema.Hii Wizara(Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)kimsingi ni dhamana yake kwasababu yeye ndio Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama,kwa msingi huo ni kwa neema ya Mungu na kwa mapenzi yake na ufunuo wake Mungu kupitia Rais wetu mpendwa, amenipa dhamana nisimame kwa niaba yake katika kuhakikisha ninakua karibu nanyi kama daraja la kuwasaidia katika majukumu yenu,katika kutekeleza sheria,taratibu lakini kufanya kazi hii ya Kimungu mkishughulika Kiroho kwa Koroani tukufu na Biblia takatifu nasi tukishughulikia Watanzania Kimwili kuleta Ustawi na maendeleo yao kupitia Katiba na Sheria,”*

*“…..Niliapa mbele ya Mwenyezi Mungu,nikaapa mbele ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuilinda na kuitetea ambayo ni ya kwetu sisi wote na nikaapa mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwamba nitafanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na kumshauri kwa hekima na busara ambayo lazima itoke kwa Mungu”amesema Katambi*




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top