Ufunguzi wa Kanisa na Harambee ya Ujenzi wa Shule na Zahanati Kijiji Cha Musati Serengeti Sasa ni Aprili 18

GEORGE MARATO TV
0

 


TAASISI ya Nyansaho Foundation imendaa harambee kubwa kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa Zahanati na Shule ya msingi ya kisasa katika kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara. 

Jaji Mkuu wa Tanzania mh George Masaju anatarajia kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu wa 2026, sambamba na ufunguzi wa kanisa la Waadventista Wasabato Musati Central. 

Imeelezwa kuwa mwenyeji wa harambee hiyo anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa taasisi ya Nyansaho foundation ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa mhe.Rhimo Nyansaho huku waziri wa ujenzi mhe. Abdallah Ulega akitarajia kuwa mgeni maalum. 

Awali ufunguzi wa kanisa Hilo jipya na harambee hiyo ulipangwa kufanyika machi 28 mwaka huu lakini ukiahirishwa baada ya kutokea kifo cha waziri William Lukuvi. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top