Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Shilingi Trilioni 1.77 Zahitajika Kukidhi Miundombinu ya Elimu Mwaka 2028


JUMLA ya sh. trilioni 1.77 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, ajira mpya za walimu, ruzuku ya mitihani, ya vitabu na uendeshaji kwa wanafunzi zaidi ya milioni tatu wanaotarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028.

Hayo yamesemwa Bungeni, jijini Dodoma leo (Jumatano, Aprili mosi, 2026) na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2026/2027.


“Tathmini inaonesha kuwa wanafunzi 3,021,177 wanatarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028. Jumla ya gharama zinazohitajika ni shilingi trilioni 1.77 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 23,226; matundu ya vyoo 46,632; maabara 9,366; ajira mpya za walimu 40,192; ruzuku ya vitabu na uendeshaji pamoja na ruzuku ya mitihani na upimaji,” amesema.

Amesema mahitaji hayo yanatokana na uamuzi wa Serikali kuimarisha sekta ya elimu kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023), mitaala iliyoboreshwa, mipango na mikakati mbalimbali ikiwa na lengo la kuzalisha rasilimaliwatu wenye ujuzi na maarifa stahiki yatakayowezesha kumudu ushindani wa ajira na uwezo wa kujiajiri ndani na nje ya nchi.


Amewataka Wakuu wa Mikoa wasimamie kikamilifu maandalizi na mapokezi ya wanafunzi wa elimumsingi ya lazima ya miaka 10 watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028 kwa kukamilisha miundombinu na huduma zote muhimu.

“Tunaposema elimu ya lazima kuwa miaka 10, kimsingi tunasema tulikuwa na sekondari kila kata, sasa tunaongelea kuwa na shule ya sekondari kila kijiji. Lazima tujiandae kwa miundombinu pamoja na maoteo ya mahitaji yote ya kutekeleza mpango huo.”

Amesema ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kuendelea na masomo, katika mwaka wa fedha ujao, Serikali imetenga sh. bilioni 139.28 kupitia mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4,193 na matundu ya vyoo 13,943. Na kupitia Serikali Kuu, Waziri Mkuu amesema, zimetengwa sh. bilioni saba kwa ajili ya ujenzi wa maabara 233.

Alielezea kuhusu ujenzi wa shule mpya za sekondari za amali, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imetoa sh. bilioni 88.84 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya 103 za amali. “Kati ya hizo, ujenzi wa shule 27 umekamilika na zinatumika. “Hadi kufikia Februari, 2026 shule 158 za sekondari ya chini (O’ level) zinatekeleza mkondo wa amali wa mitaala iliyoboreshwa ikilinganishwa na shule 41 zilizoanza mwaka 2024,” amesema.

“Ili kuboresha ufundishaji wa masomo ya amali, Serikali imepeleka walimu 150 kwenye mafunzo ya muda mfupi nchini India. Aidha, walimu 156,948 kati 172,609 kutoka shule za msingi 17,111 pia walishiriki mafunzo endelevu kazini.”

Akielezea utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/2026, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa shule mpya za msingi 277. “Serikali imeongeza miundombinu katika shule za msingi na sekondari zilizopo kwa kujenga madarasa 5,439, majengo ya utawala saba, mabweni 21, hosteli 26, nyumba za walimu 69, maabara 46, mabwalo matano na vituo vya walimu 70. 

Akifafanua kuhusu ukarabati wa shule, Waziri Mkuu amesema Serikali imekamilisha ukarabati wa shule za msingi 228 na ujenzi wa miundombinu iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ikiwemo maboma 132 ya mabweni ya shule za sekondari, vyumba vya madarasa 697 katika shule za msingi na vyumba vya maabara 175 katika shule za sekondari.

Waziri Mkuu ametua fursa hizo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka vifaa vya maabara katika shule za sekondari 231 zikiwemo shule mpya 26 maalumu za kitaifa za sayansi za wasichana.

Mbali na hilo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza Mpango wa Elimu Bila Ada kwa kugharimia elimu ya awali hadi elimu ya sekondari ya juu ambapo hadi kufikia Februari, 2026 shi. bilioni 383.22 kati ya sh. bilioni 510.96 sawa na asilimia 75 zilikuwa zimetolewa kwa shule za msingi 18,119 na shule za sekondari 5,179.

Kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe sh. trilioni 12.5 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ambapo kati ya fedha hizo, sh. trilioni 8.73 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. trilioni 3.76 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. 

Vilevile, Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe sh. bilioni 225 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya fedha hizo, sh. bilioni 207.99 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. bilioni 17.02 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...