Kanali Mtambi aipongeza Takukuru Mkoa wa Mara

GEORGE MARATO TV
0






Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 19 Machi, 2026 amefanya mahojiano ya vipindi vya televisheni vinavyoratibiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU katika Jijini Dodoma. 

Akizungumza katika mahojiano hayo Mhe. Mtambi ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Mara kwa ushirikiano wanaoutoa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Mara. 

' TAKUKURU inatusaidia sana kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, ni jicho letu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na katika ubora unaotakiwa" amesema Mhe. Mtambi. 

Mhe. Mtambi amesema kutokana na kazi inayofanywa na TAKUKURU wananchi wa Mkoa wa Mara wanauhakika wa miradi yao inatekelezwa vizuri, kupata huduma bora, kupunguza mianya ya rushwa. 



Mhe. Mtambi ametoa mfano wa TAKUKURU kufuatilia Shule ya Sekondari ya Kasoma Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo awali shule hiyo ilikuwa inatumia kuni kupika chakula lakini baada ya ufuatiliaji wa TAKUKURU na kuwashirikisha wadau wa maendeleo kwa sasa shule hiyo inatumia nishati safi ya kupikia. 

Mhe. Mtambi amewapongeza pia wananchi wa Mkoa wa Mara wanaoshiriki katika usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao. 

Mhe. Mtambi amesema wananchi wamesaidia sana katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuchangia fedha, nguvu kazi, kufanya ufuatiliaji na kutoa taarifa pale wanapoona kuna tatizo katika utekelezaji wa miradi hiyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top