Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori na Mabasi Tanzania (TLDTA), Hassan Dede amehimiza waandishi wa habari kufanya kazi kwa uzalendo kwa manufaa ya nchi yao, Tanzania.
Dede ameyasema hayo Alhamisi Machi 19, 2026 wakati wa Iftar aliyoiandaa kwa ajili ya waandishi wa habari jijini Mwanza.
Amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yao hivyo ameona ni vyema kujumuika nao pamoja kama ishara ya umoja, mshikamano na upendo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.
Naye mmoja wa waandishi wa habari jijini Mwanza, George Binagi amemshukuru Dede kwa kuthamini mchango wao kwani Iftar hiyo imeimarisha umoja na mshikamano kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa maendeleo jijini Mwanza





