Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia alivyoitoa Wizara Maji kutoka kuwa ya kero na lawama hadi ya faraja

 

Na: Dk. Reubeni Lumbagala

Maji ni miongoni mwa huduma muhimu ya kijamii. Maji ni huduma ambayo kila mtu anahitaji tena kila siku. Utahitaji maji kwa kuoga, kupikia, kufulia, kupigia mswaki, kunyweshea mifugo, kumwagilia maua au bustani. Mambo yanayohitaji maji ni mengi. Maji haya yanapaswa kusambazwa kutoka katika vyanzo vyake mathalani mito, maziwa na mabwawa hadi katika makazi ya watu ili yaweze kutumiwa. Wananchi wanataka maji yawafikie katika makazi yao, hiyo ndiyo kiu na hitaji lao.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anatoa ushuhuda wa hali ya maji iliyokuwa hapo nyuma. "Kitendo cha wananchi wa maeneo mbalimbali nchini kukosa maji kuliifanya Wizara ya Maji kuwa ni Wizara ya kero na lawama, lakini kwa kazi kubwa alizofanya Rais Dk. Samia, leo Wizara imekuwa faraja kwa wananchi," anasema Aweso. Maneno  ya Waziri Aweso yanatokana na ukweli kuwa katika maeneo mengi nchini, wananchi walikabiliwa na shida ya maji, hivyo walikuwa na lawama nyingi kwa Wizara ya Maji kwani ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kule walipo, hivyo Wizara ya Maji haikuwa na namna ya kukwepa lawama hizo.

Kutokana na utashi wa kisiasa uliopo wa serikali wa kutatua kero za wananchi ikiwemo kero ya ukosefu wa maji, serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua stahili na madhubuti kuhakikisha Wizara ya Maji inakuwa faraja kwa wananchi kwa kuwafikishia huduma ya maji na hivyo maji kuchangia maendeleo ya sekta nyingine ili kwa pamoja kasi ya maendeleo iweze kuongezeka. 

Waziri Aweso anakiri Rais Dk. Samia ameleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo kwani miradi ya maji iliyokuwa imekwama sasa inafanya kazi na maji yanatoka. Ni ukweli mtupu kuwa Rais Dk. Samia anaumizwa na shida ya wananchi kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji ambayo wakati mwingine hayana uhakika wa kuyapata. Muda wa kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi wananchi inabidi wautumie kutafuta maji  kwa matumizi mbalimbali kama ya kupikia, kufulia na kuogea.

Ndoa zilikuwa zipo njia panda. Wanandoa wanagombana kwa sababu mke amechelewa kurudi nyumbani kutoka kisimani, bombani au mtoni kuchota maji. Watoto wanachelewa kwenda shule kutokana na kutafuta maji. Rais Dk. Samia amefanya kazi kubwa kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Maji kutoka shilingi  bilioni 680.3 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi shilingi trilioni 1.01 mwaka wa fedha 2025/2026. Mapinduzi haya makubwa yamefanikisha kuongezeka kasi ya usambazaji maji kwa wananchi hali inayoleta faraja badala ya lawama.

Rais Dk. Samia amefanikisha uzinduzi wa miradi ya maji kuwa endelevu badala ya miradi hiyo kutoa maji pale tu wanapokuja viongozi kukagua na kuzindua. Uendelevu wa miradi ya maji inatoa uhakika wa wananchi kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza. Waziri Aweso anasisitiza Rais Dk. Samia kuwa kinara wa maji kwani miradi iliyokuwa imekwama tangu miaka ya 1970, sasa imekamilika na inatoa maji. Wizara ya Maji imekuwa faraja kwa wananchi kutokana na fedha za miradi kutolewa kwa wakati kugharamia miradi hiyo. Jambo la kufurahisha hapa ni kwamba, fedha nyingi za miradi ya maji ni mapato ya ndani (own sources) badala ya kutegemea misaada ya wahisani. 




Kwa mujibu wa Waziri Aweso, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia, zaidi ya shilingi trilioni tatu zimetolewa kugharamia miradi ya maji, jambo linaloongeza kasi ya usambazaji maji kwa wananchi. Katika kuendeleza tabasamu kwa wananchi, Wizara ya Maji inatekeleza mpango mkakati wa ujenzi wa Gridi ya Taifa ya Maji ili kuhakikisha maji yanakuwa ya kuhakika kwa matumizi mbalimbali ya kimaendeleo.

Katika Wiki ya Maji iliyozinduliwa Machi 16 hadi 22, 2026, Wizara ya Maji ina kila sababu ya kutembea kifuambele kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana likiwemo suala la upatikanaji wa maji kufikia asilimia 92.5 maeneo ya mijini na asilimia 85.2 maeneo ya vijijini. Kazi nzuri zimefanyika. Kwa maeneo ambayo maji hayajafika, dhamira ya serikali ni ile ile kuwafikishia wananchi wake wote maji safi, hivyo kazi ya kufikisha maji kwa wananchi wote inaendelea tena kwa kasi na viwango vikubwa.

Maoni: 0620 800 462.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...