Wananchi wa Kijiji Cha Kiriba Wajitolea Kujenga Shule ya Sekondari

GEORGE MARATO TV
0


 MARA

KATIKA kuunga Mkono jitihada za Serikali kwenye Sekta ya Elimu nchini, Wananchi wa kijiji cha Kiriba, mkoani Mara kwa Kushirikiana na Benki ya NMB,CRDB pamoja na ofisi ya Mbunge wamejitolea kujenga shule ya ufundi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwafanya vijana kuwa na Ujuzi.

Hatua hiyo imeifanya Familia ya Mashenene kuanza kujenga chumba kimoja cha darasa ikiwa ni mchango wa familia hiyo kwenye ujenzi wa sekondari hiyo ambapo Familia hiyo inaanza kupau chumba chao cha darasa wiki ijayo.

Akiambatana na Wananchi katika eneo la ujenzi huo leo March 19,2026 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo katika kuunga jitihada hizo za ujenzi wa "Mwigombe Technical Secondary School" kijijini Kiriba.

Kadhalika, Michango ya ujenzi imeshaanza ambapo imeanza kutolewa na,Wakazi wa Kijiji cha Kiriba,Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba,Mbunge wa Jimbo, Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki za NMB na CRDB.

"Sisi wananchi wa Kiriba Tunakuomba mchango wako uchangie ujenzi wa sekondari hii kupitia akaunti ya Kijiji cha Kiriba,Benki: NMB

Akaunti Na: 30302300894

Jina: Serikali ya Kijiji Kiriba". Wamesisitiza wananchi

Sambamba na hayo Ujenzi upo Kwenye Boma moja lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja umekamilika ambapo Upauaji utakamilika kabla ya tarehe 30.4.2026

Pia,Wananchi wa Kijiji cha Kiriba Mkoani Mara wanatoa shukrani nyingi sana kwa benki za NMB na CRDB kwa kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa sekondari ya ufundi ya kijijini hapo.

"Sekondari hii ikikamilika itakaribisha vijana wa kutoka vijiji vingine vya Jimboni Hilo kuchukua elimu ya ufundi itakayotolewa hapo". Wamesema wanakijiji

Hamasa hii ya Wananchi wa Kiriba kujitolea kujenga shule na michango katika sekta ya elimu ni kuunga mkono juhudi za mbunge wa Jimbo Hilo Prof. Sospeter Muhongo ambaye amejitoa kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo hasa katika sekta ya elimu katika Jimbo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top