Na Mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema mkoa wa Mara na wanawake wa Chama walitaka Jeshi la Polisi kutozuia Kongamano la Wanawake linalotarajia kufanyika Machi 8,2026 Duniani kote.
Akiongea kwa niaba ya wanawake wa Chadema Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Veronica Sando amesema haoni sababu ya Jeshi hilo kutoa tamko la kuzuia Kongamano hilo kupitia vyombo vya habari kwani wanawake wa Chadema wamejiandaa kusherekea siku hiyo.
"Siku hiyo ni siku ya wanawake Duniani kote kwa nini Kamanda wa Polisi azuie kama anazuia basi azuie pia kwa wanawake wa taasisi nyingine vikiwemo na vyama vya kisiasa sisi ni akina mama na tarehe 8 Machi,2026 tunaungana na wanawake Duniani kote kufikisha jumbe zetu, kupewa kauli kwa mdomo na kutakiwa kufika kituo Cha Polisi kwa maelezo ya mdomo hii siyo haki ni uonevu,mbona hata madhehebu ya dini wanaadhimisha kwa umoja wao wasituvuruge", amesema Veronica.
Ameongeza kuwa sababu aliyoielezea si ya msingi kwa kuwa siku hiyo ni siku ya wanawake na si wanaume wala si siku ya Chadema Tanzania, maadhimisho haya yanaadhimishwa na Dunia yote ,amesema yeye na wanawake wote wa Chama hicho hawatakuwa tayari kuacha kushiriki siku hiyo kama ndivyo vyama vyote visishiriki.
Amekiri uwepo wa kesi ya msingi mahakamani lakini amesema siku ya wanawake Duniani haihusiani na chama ni kufurahia uhuru kwa wanawake na BAWACHA mkoani hapa na Kanda yote ya Serengeti na wote nchini hawaoni haja kwa Jeshi hilo kuingilia siku hiyo kwani hata Rais.Samia Suluhu Hassan nae anasheherekea siku hiyo hivyo zuio hilo ni batili na kutisha wanawake washindwe kufurahia,amewasisitiza wanawake BAWACHA kushiriki kwa wingi na anawakaribisha mkoani hapa.
Nao wanawake wa Chadema wamesema siku hiyo ni ya wanawake Duniani kote si ya Chadema pekee hivyo wapo tayari na watashiriki kikamilifu kwa kuwa ndio siku yao ya kutoka pia ni siku ya furaha,faraja na kupigania masuala ya haki za wanawake wote bila kujali vyama vyao.
Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Pius Lutumo amesema kuwa kila mtu ana haki ya kuzungumza Jeshi la Polisi limetoa utaratibu wake na tamko lake na Chadema nao wamezungumza hivyo taratibu na Sheria zifuatwe.



