WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 22, 2026 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha.
Mradi huo unaofadhiliwa kupitia bajeti ya maendeleo ya Serikali, unalenga kuongeza uwezo wa malazi ya wanafunzi kutoka 600 hadi 1,000.
Mradi huo unatekelezwa kwa awamu tatu, ambapo kila awamu inajumuisha ujenzi wa jengo moja la bweni, ikiwemo vyumba maalum kwa wanafunzi wa kike wenye watoto au mahitaji maalum
Awamu ya kwanza ya ujenzi imepangwa kugharimu shilingi bilioni 6.10, hadi sasa fedha zilizotumika ni shilingi bilioni 4.74 na ujenzi umefikia takribani asilimia 80.









