Nyansaho Foundation Kwa Kushirikiana na Mbunge wa Serengeti Watoa Tabasamu Kwa Wanafunzi 361

GEORGE MARATO TV
0

TAASISI ya Nyansaho Foundation kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Serengeti imekabidhi vifaa mbalimbali vya masomo kwa wanafunzi 361 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 60.

Wanafunzi hao ambao wamenufaika na msaada huo wametoka kata 30 za jimbo la Serengeti ambao walishindwa kuripoti katika shule zao za Sekondari walizopangiwa kwa kukosa mahitaji hayo muhimu.


Akikabidhi Mahitaji hayo leo February 22,2026 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Bi. Mary Daniel ambaye ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo amekabidhi Msaada huo zikiwemo Shati,Sketi,Suruali,viatu,counter Book, bokei la kalamu, Rimu za kuandikia na kusomea,Rula,Kiwi za viatu, brashi pamoja na Begi.


Baada ya kukabidhi Mahitaji hayo Mhe. Mary Daniel amewasisitiza,wazazi, walezi pamoja na Wananchi Kwa ujumla kuwahamasiahana kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni ili waendelee na Masomo.

 "lakini pia niwasisitize wananchi kwamba wasaidieni sana watoto wetu kutimiza ndoto zao kwani kufanya hivi mtawasaidia sana". Amesisitiza 

Kwa upande wake Mratibu wa Nyansaho Foundation Kanda ya ziwa bi Modester Mwema,amesema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi zote za maendeleo katika wilaya hiyo,zikiwemo shughuli za kiuchumi katika kupambana na umasikini katika jamii hiyo.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top