Chuo cha Uhasibu Arusha Chaweka Mikakati Katika Kuwainua Vijana Kiuchumi

GEORGE MARATO TV
0


 DODOMA.

IMEELEZWA Kuwa Changamoto Kubwa inayowakabili vijana wengi Nchini Katika Safari ya Kujiajiri ni Ukosefu wa Elimu ya Fedha na Elimu ya Rasilimali watu.

Kutokana na changamoto hiyo katika kipindi Cha siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Kimejikita Kuwaandaa Vijana kwa kuwapatia Elimu ya Fedha na Ujuzi wa Biashara ili Waweze Kujiajiri na Kujitegemea.

Hayo yamebainishwa Leo February 20,2026 Jijini Dodoma na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Prof.Eliamani Sedoyeka, wakati wa mkutano wake na wanadishi wa habari kuhusu siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni zamu ya taasisi.


Amesema Kuwa Chuo Hicho Kimejikita Katika Kuwaandaa Vijana Kwa Kuwapatia Elimu ya Fedha na Ujuzi wa Biashara ili Waweze Kujiajiri na Kujitegemea.

"Vijana wengi wana Ujuzi wa Kitaaluma na Kiufundi, lakini Wanakosa Maarifa ya namna ya Kuugeuza Ujuzi huo Kuwa Fursa ya Ajira na Chanzo Cha Kuajiri Wengine". Amesema

Aidha Prof. Sedoyeka Amesema Chuo hicho Pamoja na Kuwa na Mitaala inayokidhi Mahitaji ya wakati ya Soko la Ajira, IAA imewajengea Uwezo Wanafunzi Kuanzisha Miradi yao Kupitia IAA Kituo Cha Kuanzisha Biashara, Ambapo Baadhi ya Wanafunzi Wameanzisha Biashara Ndogo Ndogo ambazo zinaendelea Kukua Vizuri. 

Amesema Katika Mwaka wa Masomo Ulioisha Wameweza Kuwafikia Ziaidi ya Vijana 8600 kati yao Vijana 1520 Walibuni Mawazo Mbalimbali ya Biashara na Kufanikiwa Kuanzisha Biashara zaidi ya 50 ambapo Katika hizo Kampuni 12 Zilisajiliwa.

Katika Hatua Nyingine, Amesema IAA Ni Miongoni Mwa Taasisi za Umma Zilizonufaika na Mradi wa Elimu ya Juu Kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Unaofadhiliwa Kwa Mkopo Wa Masharti Nlnafuu Kutoka World Bank Kupitia Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Chini Ya Serikali Ya Awamu Ya Sita.

Ametaja maeneo ya kipaumbele ya utekelezaji wa mradi huu tunayonufaikana nayo kama Chuo ni ujenzi na uboreshaji wa miundombinu,kufanya mapitio ya mitaala kuendana na mahitaji ya soko la ajira, kuimarisha uhusiano na sekta binafsi, kuimarisha matumizi ya teknolojia na kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na kuwajengea uwezo wafanyakazi.

"IAA ni miongoni mwa taasisi za umma zilizonufaika na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)". Amesema

"Ushirikiano wa Kisekta 

Tarehe 09 Februari 2026, Makamu wa Rais Balozi. Dk.Emmanuel Nchimbi alizindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi 

za Elimu na Sekta, wenye lengo la kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya fursa na kujenga taaluma zinazokidhi Mahitaji ya Soko la Ajira". Ameongeza 

Kadhalika amesema Kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) IAA imeunda kamati ya ushauri ya kisekta ambayo itakuwa daraja kati ya chuo na wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma. Kamati itasaidia kushauri chuo katika kuandaa na kufanya mapitio ya mitaala ili kuwa mitaala inakidhi mahitaji ya wakati ya soko la ajira.

"ili kuhakikisha tunaandaa wahitimu mahiri wenye ujuzi unaohitajika katika mazingira halisi ya kazi IAA imeingia makubaliano na kusaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano (MoUs) na baadhi ya taasisi katika sekta binafsi ikiwemo CEOs Round Table, ambazo zitatoa fursa kwa wanafunzi wetu kujifunza na kupata uzoefu wa mazingira ya kazi". Amesema 

Mkuu huyo amesema ushirikiano huu utatoa fursa ya ushiriki wa sekta ya binafsi katika ufundishaji na ujifunzaji; mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa kwa mfumo rasmi (internship), mafunzo ya vitendo kazini (field attachment); fursa za wanafunzi kujifunza uongozi kupitia wataalam wa vitendo, tafiti zinazohusisha changamoto halisi za biashara na uchumi pamoja na ubadilishanaji wa maarifa kupitia mihadhara ya umma na mijadala shirikishi.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top