Zaidi ya wakazi 22,482 Misungwi kupata huduma ya maji safi, wamshukuru Rais Dkt Samia

GEORGE MARATO TV
0




Zaidi ya wakazi 22,482 wa Mji wa Misungwi wanatarajiwa kuanza kunufaika na mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ambao sasa umefikia hatua za majaribio.

Mradi huo unahusisha ulazaji wa mtandao wa bomba kwa urefu wa KM 38, ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji (Lita 150,000 na Lita 90,000), ujenzi wa kituo cha kusukuma maji kinachojengwa pamoja na Kisima cha maji (Sump well - Lita 50,000) na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji (domestic points).

Mradi umetekelezwa na MWAUWASA kupitia Mkandarasi kampuni ya DATTI CONSTRUCTION LTD kwa fedha kutoka Wizara ya Maji kiasi cha TZS Milioni 888 na utanufaisha wakazi wa maeneo ya *Mbela B, C na D, Shule ya Sekondari Mbela, Mitanda, Mwambola, Ng'ombe, Iteja, Old Misungwi na Mwamanga.*

Hatua ya majaribio inayoendelea kwa sasa inalenga kuhakikisha mifumo yote inafanya kazi kwa ufanisi kabla ya kuanza kutoa huduma rasmi kwa wananchi.

Kukamilika kwa mradi huu kunaenda kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo na kufikisha asilimia 97% za upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Misungwi


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top