Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amemjulia hali mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Ibrahim Shayo ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Ibrahim alipata ajali Februari 18, 2026 katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.


