Makamu wa Rais Balozi Nchimbi kuweka Jiwe la Msingi Wiki kesho Jumatatu Disemba 15, 2025._
Licha ya Mkoa wa Kagera kusifika kwa usomi lakini hadi muda huu hakuna Chuo Kikuu, ni mwaka jana 2024 Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilianza kujenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tawi la Bukoba kwa gharama ya Bilioni 13.1. Ujenzi unaendelea vyema ukiwa zaidi ya asilimia 78. Chuo hiki kinajengwa kwenye Kijiji cha Itawa, Kata ya Karabagaine Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini ili kuwezesha sasa vijana na wananchi wapate elimu ya juu ndani ya Kagera.
Makamu wa Rais wa Tanzania Balozi Emmanuel Nchimbi wiki ijayo Jumatatu 15/12/2025 kuanzia Saa 1 asubuhi ataweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Chuo hicho.
Serikali ya Rais Samia imedhamiria kufanya mageuzi ya maendeleo na ndiyo maana miradi mikubwa kama hii ya Vyuo Vikuu vinajengwa hadi pembezoni kabisa katika nchi ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Wananchi wote wanakaribishwa kwenye tukio hili muhimu kwenye mkoa.



