Makamu wa Rais Dkt Nchimbi amlilia Mhagama

GEORGE MARATO TV
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Taifa limepata pengo kuondokewa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Jenista Mhagama ambaye alikuwa kiongozi aliyeheshimika na kutumikia nchi katika majukumu mbalimbali ya kitaifa.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi alipowasili kuhani msiba nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Mhagama eneo la Itega Jijini Dodoma. Amesema ripoti Mhagama licha ya kuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, lakini pia alitoa mchango wake katika Chama Cha Mapinduzi na maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia na waombolezaji na kuwaombea watoto wa marehemu na ndugu wa karibu, Mungu awape ujasiri wa kukubali jambo hilo na kutambua ni njia ya watu wote.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top