Mkurugenzi Mkuu wa Msama Promesheni Ndugu, Alex Msama amempongeza Mgombea wa Urais Kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kampeni zake alizozifanya Ndani ya Mwezi Mmoja bila kupumnzika huku akisema ameonyesha ukakamavu wa hali ya juu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kinondoni Jijini Dar es Salaam Msama amesema Mapokezi makubwa waliomuonyesha Wananchi Mikoani ni ishara yakuwa Atachaguliwa na kushinda kwa kishindo.
Aidha Msama amewapa onyo wale wote wanaondelea kutoa lugha za matusi mitandaoni kuacha mara moja huku akiwasihi watanzania kuwapuuza watu hawa huku akidai wanatumika na mabeberu wasiokuwa na nia njema na Taifa la Tanzania huko nje ya nchi.