Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam kupitia Chama cha ACT Wazalendo Glory Tausi ametembelea Soko la Kawe lililoungua moto na kuteketeza kwa kiasi kikubwa bidhaa na mali za wafanyabiashara wa soko hilo.
Tausi amekutana na baadhi ya wafanyabiashara mmoja mmoja na kutoa pole za dhati kwa niaba ya wote walioathiriwa na tukio hilo la kusikitisha.
Mgombea huyo pia ametoa pole kwa Afisa Mtendaji wa kata ya kawe
Aidha amewaomba wakazi wote wa Kawe kushirikiana kwa pamoja katika kuwafariji na kuwasaidia wenzetu waliopoteza mali na riziki zao kufuatia tukio hilo.
"Kwa pamoja tukisimama tunaweza kuwasaidia waathirika kurejea kwenye shughuli zao na kuendelea kupambana kwa ajili ya maisha bora" Alisema Tausi
Soko lililoteketea kwa moto halikuwa linatoa huduma kwa wakazi wa Kawe pekee, bali pia lilikuwa msingi wa kipato na riziki ya kila siku kwa wananchi na wafanyabiashara wa eneo hilo.
"Hivyo, nipo pamoja nanyi kwa kila hatua wananchi wenzangu wa Kawe katika kipindi hiki kigumu" Alihitimisha Glory Tausi,Mgombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia ACT Wazalendo katika Taarifa yake kwa Umma.