Na Angela Sebastian
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Bakoba vijijini Mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk
Jason Rweikiza ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 6,465 akifuatiwa na Faris Burham kura 4619.
Akitangaza Matokeo hayo, Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba vijijini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jesca Ndyamukama amesema kuwa kura zilizopigwa ni 11,682 kura halali 11,582 na zilizoharibika ni kura 100
Katibu huyo amewatangaza Wagombea wengine ambao ni Fahami Mastawili kura 239,Asted Mpita kura 124,Edmund Rutaraka kura 89 na Philibart Bagenda kura 44.