Uongozi wa Shule za Kaizerege Wamshukuru Rais Samia

GEORGE MARATO TV
0


Na Angela Sebastian; Bukoba 

UONGOZI wa shule za Kaizirege na Kemebos zilizopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamemshukuru Dk.Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya kugharamia masomo ya elimu ya juu ndani na nje ya nchi, wanafunzi wanne wa shule hiyo waliohitimu kidato cha sita mwaka huu kati ya 50 wa mchepue wa Sayansi nchi nzima.

Wanafunzi hao waliopata matoke ya daraja la kwanza la alama tatu katika mchepuo wa Sayansi ni Anitha  Kulwa aliyekuwa akisoma PCM,Bright Yohana PCB pia Christopher Wambura na Cleophas Wambura ambao ni watoto mapacha waliosoma PCB.

Wakato huohuo uongozi wa shule hiyo umetoa tuzo yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa wanafunzi hao kama motisha na pongezi kwa matokeo hayo.

Mkurugenzi wa shule za Kaizirege na Kemebos Eusto Ntagalinda akikabidhi tuzo hizo jana shuleni hapo Minispaa ya Bukoba ambapo alimshukuru Dk.Samia kwa kutoa ufadhili huo wa masomo kwa vijana hao wanne ambao walikuwa wakisoma mchepuo wa Sayansi hari itakayosababisha wengine kuiga mfano huo wa kufanya bidii katika msomo na kupata matokeo mazuri.

Akikabidhi tuzo hizo Ntagalinda amesema alianzisha tuzo hiyo kwa ajili ya wanafunzi wanaofanya vizuri katika matoke ya kidato cha sita na kuingia 10 bora kwa lengo la kuweka hamasa kwa wanafunzi wote ili waweze kusoma kwa bidii, kupata matokeo mazuri na ya heshima. 

"Kwanini ninaamua kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri siyo kwamba nina fedha nyingi bali ni kuhamasisha wanafunzi wote wanaosoma hapa kusoma kwa bidii,yawezakana hii tuzo ndiyo iliyowaongezea nguvu ya kusoma na kupata matokeo mazuri ambayo yametuheshimisha sisi,wao na Taifa letu"ameeleza Ntagalinda. 

Amesema watoto hao wameishavuna mengi wameua ndege wengi kwa jiwe moja ambapo ufaulu wao wa juu umewapatia zawadi ya kila mmoja kupata shl mil tano pia kutokana na taarifa nilizopata kutoka kwa mkuu wa shule kuwa wanafunzi hao wamepata ufadhili na si mkopo bali watasomeshwa na Serikali bure elimu yao ya juu.

Amesema kuwa mtoto anapofauru masomo yake vizuri ni furaha na fahari kwa wazazi,jamaa na ndugu hivyo ata hawa wameishapata zawadi nyingi tangu matokeo yalipotangazwa ikiwemo kwenda kusoma bure na kupitia kujituma kwao wataweza kupata nafasi nzuri za kazi Serikali pindi watakapo maliza masomo ya elimu ya juu. 

Aidha amewashauri wanafunzi walioko katika madarasa ya mitihani kujituma na kusoma kwa bidii,kutumia muda mwingi kwenye masomo kwasababu wamekwenda shuleni kusoma na si vinginevyo,kwani wanatofautiana kiuwezo wa darasani kwani binadamu hawalingani hivyo linalowezeka kwa wakati huo lisingoje kesho watumie muda wao vizuri kusoma.

"Wanafunzi waliobaki jiepushe na makundi yasiyofaa na jiwekeeni malengo ya kufanya vizuri katika masomo yenu na kupata matokeo mazuri maana mimi mkurugenzi wenu nipo tayali kuendelea kutoa zawadi kwa kila atakayekudhi vigezo na sitajali idadi ya wanafunzi hivyo nipimeni kwa kufauru ndipo mtanifahamu kuwa naguswa na matokeo mazuri "ameeleza mkurugenzi. 

Kwa upande wa mkuu wa shule hizo mwalimu Kishe Ilamulira ameeleza kuwa wanafunzi hao watagharamiwa masomo yao ya vyuo vikuu na Rais Dk. SamiaSuluhu Hassan,ambapo Anitha atakwenda kusoma nje ya nchi kwani amekuwa mwanafunzi wa tatu kitaifa kati ya wanafunzi 50 wa mchepuo wa Sayansi wenye hesabu ndani yake huku Bright,Christopher na Cleophas watasoma vyuo vikuu vya ndani ya nchi.

Amesema tuzo hizo zinaongeza molali kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa.

Kwa upande wa wanafunzi hao wamesema siri ya mafanikio yao katika kupata ushindi  shuleni  hapo ni kuomba Mungu, kujiwekea malengo,kusoma kwa bidii,kujiamini,ushirikiano, kujikubali na kujifunza vitu vipya na kuheshimu kila mmoja kwa nafasi yake na kijituma.

Anitha Kulwa ni mmoja wa wanafunzi hao amesema shule yao inatayalisha wanafunzi kwa kutoa elimu bora,kuwajengea vipaji na kujiamini ambapo mambo hayo huwasaidia katika kutujengea uwezo wa kujiamini popote wanapokwenda,kuendelea kuwa vinara katika mitihani yao na kujijengea heshima ya pekee wao na Taifa kwa ujumla.

Bright,Christopher na Cleophas wamemshukuru Rais Dk Samia kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafadhili watoto wanaofanya vizuri katika mitihani yao kwamba imekuwa kichocheo cha wanafunzi kujituma na kusoma kwa bidii ili waweze kupata nafasi hiyo.

Nao wazazi wa wanafunzi hao wameishukuru Serikali na Uongozi wa shule za Kaizirege na Kemebos kwa tuzo hizo na ufadhili wa masomo kwa watoto wao huku wakiwashauri wanafunzi wengine kusoma kwa malengo ili kufikia malengo yao ya kupata matokeo mazuri. 

Juliana Maguzu ni mama mzazi wa Anitha amewashauri wanafunzi hao kutobweteka huko waendako kwasababu bado wanayo kazi kubwa mbele yao hapa wamejenga msingi bado kukamilisha nyumba pia akawataka waliobaki hasa madarasa ya mitihani kutambua kuwa bila elimu maisha hayaendi,hivyo wasome kwa bidii.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top