Na Angela Sebastian ;Kyerwa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Khaldi Mussa Nsekela ameongoza kura za maoni katika jimbo la Kyerwa kwa kupata kura 5693 kati ya kura 8,134 zilizopigwa.
Katibu wa CCM Wilaya hiyo Kisamba Kisando ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi akitangaza matokeo hayo amewataja wagombea wengine kuwa ni
Innocent Bilakwate aliyekuwa mbunge kwa awamu iliyopita ambaye amepata kura 1567,Stephen Katemba kura 542 na Maxson Barthazary kura 152.
Amewataja wengine kuwa ni Benedicto Mutungilehi kura 101 na Sperata Marco aliyepata kura 16 .
Amesema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 8420 waliojitokeza kupiga kura ni 8134 zilizoharibika ni kura 63 na kura halali ni 8071 hivyo kumfanya Khald Nsekela kuongeza katika uchaguzi huo.