Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Ndugu Alex Msama ambaye alitia nia Ubunge Kupitia CCM katika Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam amempongeza Ndugu Jerry Silaa kwa kuibuka mshidi wa kura za maoni katika jimbo hilo.
Msama amesema Silaa ni rafiki yake, ndugu yake, mdogo wake na wamefahamiana kwa muda mrefu, hivyo kushindana kwao katika siasa sio uadui bali ndio ukomavu wa Demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi na Taifa kwa ujumla na ameahidi kushiriki kumpigia Kampeni.
Aidha, amewataka wote ambao majina yao yalikatwa na ambao hawajashinda kura za maoni, kusahau yaliyopita na kuwaunga mkono walioshinda na kuhakikisha CCM inashinda kwa Kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba.