Chuo Kikuu Cha Makerere Kugeuza Hosteli zake Kuwa Hoteli wakati wa Likizo

GEORGE MARATO TV
0

 Chuo Kikuu cha Makerere kimepanga Kugeuza Hosteli zake kuwa Hoteli wakati wa Likizo ya Wanafunzi ili kuongeza Mapato ya chuo hicho kikongwe zaidi Afrika Mashariki. 

Mpango huo umebainishwa Julai 25,2025 na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Barnabas Nawangwe wakati wa Makabidhiano ya Moja ya Hosteli iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na wa kisasa. 


"Nadhani tunatumia vibaya Hosteli hizi,kwanini zikae bila kutumika kwa miezi yote mitatu wanafunzi wanapokuwa Likizo bila kuzalisha fedha ilhali Hosteli zetu ni Bora kuliko hata baadhi ya Hoteli" Alisema Profesa Nawangwe wakati wa Makabidhiano hayo. 

Profesa Nawangwe amesema kuwa Chuo hicho kitashirikiana na wafanyabiashara pamoja na kampuni yake ya Makerere Holding Ltd kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa hosteli hizo Kibiashara wakati wa Likizo.


"Kwanini tusizigeuze hoteli wanafunzi wetu wanapokuwa Likizo, Watu wenye Mikutano wawe wanaleta washiriki hapa kupata huduma ya Malazi,pia wanaweza kufanyia Mikutano yao hapa na kutupatia fedha" Aliongeza 

Aidha amesema Chuo kitaachana na Utamaduni wa kuwataka wanafunzi kuja na magodoro na badala yake Magodoro yatanunuliwa na Chuo na kukodisha kwa wanafunzi ili kuongeza mapato.



Hosteli iliyokarabatiwa ya Mary Stuart ni moja ya hosteli kongwe za Wanafunzi wa kike kwenye Chuo kikuu cha makerere na kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 521.

Ukarabati huo umetekelezwa na Shirika la kitaifa la biashara linalomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF)kufuatia Maelekezo ya Rais Yoweri Museveni. 

Ukarabati wa Hosteli ya Mary Stuart ulitanguliwa na Ukarabati wa Hosteli ya Lumumba ikiwa ni Mkakati wa Serikali wa kuimarisha miundombinu ya Chuo kikuu cha Makerere, kwa lengo la kuifanya miundombinu hiyo kuwa ya kisasa zaidi.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top