Waziri Aweso Ambana Mkandarasi wa Mradi wa Maji Wilayani Karagwe

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian; Karagwe

Waziri wa maji Jumaa Aweso amewaagiza wakandarasi wa kampuni ya AFCON wanaotekeleza mradi wa kimkakati wa miji 28 wa Rwakajunju kubadili utendaji wake na kufanya kazi usiku na mchana ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji kwa wakati kuendana na malengo ya Serikali.

Waziri Aweso ametoa maagizo hayo julai 25,2025 wakati alipofanya ziara maalum ya kukagua mradi wa kimkakati wa miji 28 uliopo kata Nyabiyonza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Aweso Aweso amesema kuwa tayari Rais Samia katoa fedha kwa ajili ya mradi huo hivyo hakuna wakandarasi kuweka visingizio bali wachape kazi usiku na mchana ili kuwaondolea changamoto ya maji waliyokuwa nayo kwa muda mrefu wananchi wa wilaya hiyo.

 "Utendaji wa kazi lazima wa ubadilike hakikisheni mnafanya kazi usiku wa mchana na mradi huu ukamilike mwezi septemba mwaka huu kama mkataba unavyowataka,fedha ipo wananchi wa Karagwe wanahitaji maji safi,salama na bora siyo maneno" amesema Aweso 

Amesema kuwa pamoja na mradi huo kutumia fedha nyingi lazima wakandarasi washughulikie changamoto za vibarua ikiwemo kuwapa mikataba na malipo yao kwa wakati.

Amemtaka mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer kuhakikisha anasimamia suala la vibarua ili vijana wasipate changamoto kupata maslai yao kwani inaweza kusababisha wakaingiwa na tamaa na kudokoa vifaa vya mradi.

Aidha amewasihi wakandarasi hao kuhakikisha wanazingatia maagizo ya Rais Samia katika upande wa eneo la kutibu maji ili wananchi wapate maji Safi salama na bora.

Wakati huohuo amemteua msimamizi wa mradi wa Rwakajunju kutoka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Wilaya ya Karagwe Mhandisi Magrethi Nyange kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji ambapo katibu mkuu wa wizara hiyo Mwajuma Waziri atampangia majukumu.

Amesema uteuzi huo umetokana na utendaji na usimamizi mzuri katika mradi huo wa kimkakati wa Rwakajunju ambao umefikia asilimia 64 huku utandazaji wa miundombinu ukifikia asilimia 36 kati ya 38 zilizolengwa kwa awamu hii.

Naye Mhandisi Nyange alisema mradi huo wa miji 28 umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 60 ulianza kimkataba April 11, 2023 una unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu unatarajiwa kuhudumia kata 13 za Wilaya ya Karagwe.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top