Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Comoro Mhe. Nour el Fatih Azali ambapo wamezungumzia masuala kadhaa ya ushirikiano wa Tanzania na Comoro.
Balozi Yakubu alitumia fursa hiyo kumuelezea kusudio la ubalozi la kufanya kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji mwezi ujao kwa ushirikiano na Serikali ya Comoro katika maeneo ya Uzalishaji, Ujenzi na Tehama.
Aidha, Balozi Yakubu aliwasilisha pia masuala kadhaa ya kufanyiwa kazi na Serikali ya Comoro ambapo Katibu Mkuu Kiongozi Fatih aliyapokea na kuahidi kufanyiwa kazi.
Bwana Fatih pia alimueleza Balozi Yakubu kuwa mwaka huu Taifa la Comoro litasherehekea miaka 50 ya uhuru na matukio kadhaa yamepangwa kufanyika na wanatarajia ushiriki wa Taasisi kadhaa za Tanzania.
Mkutano huo ulifanyika katika viunga vya Ikulu ya Comoro.







Comments
Post a Comment