Na Angela Sebastian ;Bukoba
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa magari 14 mapya kwa jeshi la polisi mkoani Kagera kwa kipindi cha mwezi Januari hadi sasa lengo likiwa ni kuimalisha utendaji kazi na kuhakisha wanafanya kazi kwa weledi na kuwafikia wananchi kwa wakati popote walipo.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa jeshi hilo mkoani humo Blasius Chatanda wakati akikabidhi magari sita kati ya hayo yaliyotolewa kwa makamanda wa polisi wa Wilaya za mkoa huo leo mjini Bukoba ambapo, amesema mkoa huo si salama tena kwa waharifu kufanya vitendo viovu maana jeshi hilo limejipanga kukabiliana nao kikamilifu.
"Tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. Samia katufanyia makubwa tunayo kila sababu ya kumshukuru ni kwa mara ya kwanza, katika historia polisi mkoa wa Kagera kupata magari 14 kwa kipindi cha miezi mitatu hivyo hii inaashiria usalama mkubwa kwa wananchi mkoani humu"ameeleza Chatanda
Amesema wananchi wanalidai jeshi hilo katika kuhakiksha maisha yao na mali zao zinakuwa salama kwasababu magari hayo yametokana na kodi za wananchi hivyo,wanawahakikishia kuwa watapata matokeo chanya ambao wanayatarajia kutokana na uwepo wa usafiri huo.
Amesema kwa sasa mapori,barabara pote patakuwa salama hata wakati huu ambao tunaelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu wananchi watapiga kura kwenye mazingra yenye amani,pia wataendelea kuzalisha katika mazingira yenye usalama ambapo polisi wanaendelea kuyaweka kupitia Serikali ya Dk.Samia.
Amesema magari saba yaliishatolewa na miezi mitatu iliyopita na kukabidhiwa kati Wilaya husika na leo wamepokea magari mengine saba na kufikia magari 14 sasa.
Wakati huohuo Kamanda Chatanda amesema kutokana na uwepo wa magari hayo mapya ambayo yamewezesha jeshi hilo kufanya dolia za mara kwa mara Katika barabara zote za mkoa huo,kwa kipindi cha Januari hadi sasa hakuna matukio makubwa ya ajali za barabarani hasa za vifo ambazo zilikuwa tishio kwa mwaka jana.
"Polisi wanapokuwepo barabarani kwa wingi inasaidia kuwakumbusha madereva wajibu wao pindi wanapojisahau mfano, ukiachana na doria kwasasa tunachukua hatua kali kwa madereva ambapo kuanzia Desemba mwaka jana mpaka sasa madereva 95 wa mkoa huu wamefungiwa leseni kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani hivyo hii imesababisha walio wengi kuchukua tahadhari wanapokuwa kazini"ameeleza Chatanda.






Comments
Post a Comment