ANAANDIKA MBUNGE ANTHONY MAVUNDE
Mwaka Jana nilialikwa kwenye shughuli ya Umoja wa Wafanyabiashara wa Mboga mboga na Matunda wa Masoko (UWAWAMA) wakati wa uzinduzi huo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa UWT Ndg. Mary Chatanda.
Nikiwa hapo niliwaahidi wakina mama hawa wa UWAWAMA kuwapatia mradi wa kuinua mfuko wao kwa kuchangia cha Tsh 10,000,000 na kuwanunulia Shamba la Zabibu.
Niliwakabidhi shamba lililopo katika eneo la Mpunguzi-Dodoma na wakaanza kulima mara moja pasipo kuchelewa.
Leo ninafuraha kubwa kuona zao la kwanza la Zabibu kutoka kwenye shamba la UWAWAMA.
Nawatakia heri ya siku ya WAKINAMAMA WOTE DUNIANI







Comments
Post a Comment