Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuanzishwa kwa Majimbo mapya Manane ya uchaguzi nchini.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele ameyataja Majimbo mapya kuwa ni Kivule,chamazi,Mtumba,Bariadi Mjini, Chato Kusini,Katoro,Uyole pamoja na Jimbo la Itwangi
Jaji Mwambegele amesema kuwa Jimbo Jipya la Kivule limeanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Ukonga,Chamazi limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala.
Jimbo la Dodoma Mjini Limezaa Jimbo la Mtumba,Bariadi Mjini limetokana na kumegwa kwa Jimbo la Bariadi,Chato Kusini limetokana na Jimbo la chato,Katoro limemegwa kutoka Jimbo la Busanda,Uyole limetoka Jimbo la Mbeya Mjini huku Jimbo la Solwa likizaa Jimbo Jipya la Itwangi.
Mbali na Majimbo mapya manane,Kata mpya Tano pia zimeanzishwa nchini.
Aidha Tume hiyo imetangaza kubadilishwa kwa Majina ya Majimbo 12 ya uchaguzi ikiwemo Jimbo la Chato ambalo sasa litaitwa Chato Kaskazini,Jimbo la Singida Mashariki sasa litajulikana Ikungi Mashariki,Singida magharibi(Ikungi Magharibi)Singida Kaskazini(Ilongero) Nkenge(Misenyi) Bariadi (Bariadi Vijijini) Manyoni Mashariki(Manyoni) Manyoni Magharibi (Itigi) Tabora Kaskazini (Uyui)

Comments
Post a Comment