Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kanisa Anglikana Lasisitiza Umuhimu Wa Uchaguzi Mkuu Oktoba


📌 Askofu Mkuu Maimbo Mmdolwa ahimiza katiba ifuatwe

 ðŸ“Œ Dkt. Biteko asema milango ya Serikali iko wazi kwa mazungumzo

📌 Asema Serikali inathamini mchango wa kanisa kwa jamii


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Maimbo Mmdolwa amewahimiza Watanzania kushiriki katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 na kuongeza kuwa nchi inaweza kuingia katika mgogoro mbaya wa kikatiba kama watasikiliza watu wanaotaka kuahirisha Uchaguzi Mkuu.

Askofu Mmdolwa amesema hayo Mei 11, 2025 jijini Mbeya  katika ibada ya kuwekwa wakfu Canon Jacob William Kahemele kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi.

“ Kwa kuwa Naibu Waziri Mkuu uko hapa na tuliombe Taifa zima kutoahirisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa kuwa tutaingia katika mtanziko mkubwa na mgogoro wa kikatiba. Kama kuna changamoto zitafutiwe suluhu ziishe,”

Askofu Mmdolwa ameipongeza Serikali kwa ushirikiano wake na Taasisi za dini nchini na kuunga mkono Uhuru wa kuabudu ikiwa na lengo la kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema milango ya Serikali iko wazi chini ya uongozi wa wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwasihi wenye hoja kujongea kwa mazungumzo.

"Ninachoweza kusema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge  na madiwani  unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa uhuru na wa haki huku nchi ikiendelea kuwa na amani.

“ Uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki kama katiba inavyotaka, waliposikika waliotaka marekebisho ya sheria Serikali ilipitia na kufanya  marekebisho ya sheria zinazosimamia  uchaguzi na leo milango ya Rais Mhe. Dkt. Samia ipo wazi kwa yeyote mwenye kutoa malalamiko yake ili nchi iende mbele,” amesema Dkt. Biteko.

Amewaasa Watanzania kuendelea kuiombea nchi ili amani iendelee kuwepo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Dkt. Biteko  amesema Serikali inathamini  mchango wa madhehebu yote ya dini, ikiwemo Kanisa la Anglikana. Katika nyanja za elimu, afya, maji, na maendeleo ya jamii, Serikali inashirikiana kwa karibu na taasisi za dini kwa lengo la kuimarisha huduma kwa wananchi.

Akitoa mfano  wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini yenye makanisa 37 yanayosimamiwa na parish katika mikoa ya Songwe na Mbeya kupitia makanisa hayo yanasaidia kufikisha huduma ya kiroho kwa jamii.

“ Kuanzia mwaka 2016 hadi 2025 Kanisa kwa kushirikiana na wadau limetumia zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuendesha miradi ya “Dreams na Archive” kwa kusaidia Elimu Maalumu ya Vitendo ya kujikomboa Kiuchumi na Afya kwa Mabinti na Watoto wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI katika maeneo ya Mbeya, Songwe na Tunduma,” amesema Dkt. Biteko.

Ambapo miradi hiyo imesaidia zaidi wananchi 160,000 waliokuwa na changamoto hizo za kijamii na kiuchumi. Aidha, imejiri zaidi ya watu 150 hivyo kuwaongezea kipato na kuwarahisishia maisha wananchi.

Pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana Kanisa la Anglikana  kwa karibu zaidi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Vilevile, Dkt. Biteko amempongeza Askofu Kahemela katika safari yake mpya ya kiutumishi huku akitoa wito kwa waumini wa Kanisa hilo kumtunza na kumsikiliza Askofu huyo pamoja na kumtia moyo kuwavumilia waumini wake endapo changamoto zitatokea.


“ Tunakupongeza kwa moyo wa kujitoa kwa Mungu, kwa utii wako kwa wito wa kiutumishi, na kwa maono yako ya kiroho.

Serikali inapenda kukupa uhakika kuwa tutaendelea kushirikiana kwa karibu na Dayosisi hii chini ya uongozi wako, kwa lengo la kukuza ustawi wa wananchi wetu, kulinda tunu zetu za taifa, na kuimarisha mshikamano wa kijamii na kitaifa,” amebainisha Dkt. Biteko.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika amewaomba waumini wa kanisa la hilo kuwa na umoja  na mshikano mara baada ya uchaguzi wa Askofu wa Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini na kutii viongozi wa dini ili kuendeleza kazi ya Mungu.

Aidha, amesema Serikali iliyopo ni sikivu na endapo kuna malalamiko  yasikilizwe, na kuwa Uchaguzi usitenganishe Watanzania  bali uwaaunganishe, pia amewataka watu  wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali wafanye hivyo kwa kufuata utaratibu.

Awali akihubiri katika ibada hiyo, Mhashamu Askofu Sospeter Ndenza amesema kuwa Askofu ni Kuhani Mkuu na Mchungaji Mkuu kwa niaba ya Kristo na anasimamia nidhamu ya kanisa na kuona ibada zinasimamiwa na kufuata taratibu za kanisa pamoja na kusimamia utoaji wa huduma za sakrementi tofauti.

Amesema  wajibu huo ni mzito unahitaji uongozi na hekima ya Mungu.

“ Jacob unahitaji kumuomba Mungu akupe hekima hasa katika dunia ya leo, leo unapokusidia kuwekwa wakfu unahitaji hekima na adili ili umwakilishe kristo,” amesema Mhashamu Askofu Ndenza.

Amesema Askofu huyo asiogope vitisho kwa kuwa kutakuwa na watu watakao mpinga hata hivyo asitetereke badala yake ajue njia za Mungu na asitumie akili zake bali ajinyenyekeze kwa Mungu naye atamsaidia.

Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini, Canon Jacob William Kahemele ameahidi kuwaombea viongozi wa Serikali ili waweze kuiongoza nchi kwa amani na utulivu.

“ Wakati wa uongozi wetu tutahimiza sana watu kusali sana ili kukua kiroho kwa kuwa shetani mjanja sana na anadanganya watu kufuata njia za udanganyifu. Pia tutasisitiza 

sana uamsho wa kiroho ili watu wasiwe wachanga na kuyumbishwa huku na huko,” amesema Askofu Kahemele.

Amesema wanaamini wameitwa kufanya majukumu makubwa kwa kutoa ibada, kutenda kazi kwa uaminifu sambamba na kusaidia wenye uhitaji. 

Aidha, ametaja baadhi ya changamoto zinazowakumba  vijana nchini za matumizi ya pombe kali, sigara na michezo ya kamari hivyo ameiomba Serikali kuzuia uholela wa uuzaji wa pombe kali na sigara.

Licha ya hayo ameipongeza Serikali kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati mfano treni ya kisasa (SGR) na kuiomba kufikiria namna ya kuunganisha Mkoa wa Mbeya na Dar es salaam kwa kutumia treni hiyo ya kisasa ili kusaidia kukuza uchumi wa mkoa huo.

Ibada hiyo ya kumuweka wakfu Canon Jacob William Kahemele kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Akson, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. 







Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...