_Aongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama. Asema Rais Samia amedhamiria kumaliza changamoto ya maji kila mahali._
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mhe. Erasto Sima amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kumaliza changamoto ya maji wilayani Bukoba kwa jinsi inavyotekeleza miradi mikubwa kila mahali huku akiwataka wananchi na viongozi kutunza vyanzo vya maji ili miradi hiyo iwe endelevu.
DC Sima ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 20, 2025 akiongozana na Kamati nzima ya Ulinzi na Usalama kwenye ukaguzi wa miradi ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenye Tarafa ya Katerero, Rubale na Bugabo. DC Sima na Kamati wamefanya ukaguzi wa miradi 5 ya maji inavyotekelezwa na mingine ambayo wananchi wameanza kupata huduma ya maji kupitia usimamizi wa RUWASA.
Kwenye ziara hii, DC Sima na Kamati ya Ulinzi na Usalama wamekagua mradi wa maji wa Kata ya Katoro na Bujugo kwenye Tarafa ya Katerero, mradi wa Migara na kuzungumza na viongozi wa Jumuia za watumia maji (CBWSO) katika Kata ya Butelankuzi Tarafa ya Rubale na kumalizia jioni ukaguzi wa mradi wa maji Bumai na Bushasha kwenye Tarafa ya Bugabo.
DC Sima na Kamati nzima maeneo yote aliambatana na Maafisa Tarafa wa Tarafa husika, madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na viongozi wengine

.jpg)





Comments
Post a Comment