Na Hamida Ramadhan - Rukwa.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Deus Sangu ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akifanya Mikutano ya Kimkakati ya kumuunga mkono Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuwachagua Viongozi katika Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui na Muze zilizopo katika Jimbo la Kwela, Mkoani Rukwa.
Amesema CCM ina kila sababu ya kushinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jinsi ilivyo jipambanua kushughulikia kero zinazowakabili Wananchi wa Jimbo hilo.
Ameendele kusema kuwa, Wananchi wa Jimbo hilo wana kila sababu ya kuwapigia kura Viongozi wa Serikali za Mitaa waliogombea kupitia chama hicho ikiwa ni ishara ya shukrani kutokana na mabilioni ya fedha ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayoyatoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo.
" Tumejiandaa vilivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha tunashinda kwa kishindo " amesisitiza Mhe. Sangu
Amebainisha kuwa, katika kipindi chake cha Uongozi Mkoa wa Rukwa hususani Jimbo la Kwela limefunguka ambapo kila kona barabara zimeboreshwa huku zingine zikiendelea kuwekwa lami ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Huku, huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, umeme pamoja maji zimeimarika ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Diwani wa Muze, Mhe. Kalolo Ntalli amesema kwa jinsi walivyojipanga kutokana na ubora wa wagombea waliopitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakika ushindi ifikapo tarehe 27 Novemba mwaka huu hauepukiki.







Comments
Post a Comment