Ofisa habari wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) David Edward amesema kuwa mafunzo wanayotoa kwa sasa na wanayotarajia kuyatoa katika vyuo vingine hapa Nchini yataenda kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajali ambazo zimekuwa zikisababishwa na madereva hao wa bodaboda.
Edward ameyasema hayo Jijini Mwanza wakati akizungumza na Jambo digital na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatamsaidia dereva huyo kujua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhibiti mwendo hali ambayo itawasaidia kuzijua sheria za usalama barabarani.