Na Helena Magabe Watetezi tv.
Meneja mahusiano wa Mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara Francis Uhadi amesema kuwa kitengo chake cha mahusiaano kinatetea haki za Binadamu licha yakuwa lawama nyingi zimekuwa zikiwaangukia.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jana Octoba 11,2024 alisema kitengo cha mahusiano na wote walioajiliwa katika kitengo hicho ni watetezi wa haki za binadamu na kwa upande wake migodi yote aliyofanya kazi alikuwa akitetea haki za binadamu ila Kwa Mgodi wa north mara wamekuwa wakitupiwa lawama ambazo hawastahili.
Alisema asilimia 51 ya ajira katika Mgodi huo ni Wananchi kutoka Mara na wanatokea Nyamongo na Tarime ikiwa ni pamoja na kuajiri walinzi shirikishi 560 kutoka maeneo ya jirani na mgodi hivyo wanazingatia ajira kwa Wazawa.
Meneja Mkuu wa Mgodi huo Aporinaly Lyambiko alisema kwa Sasa kuna ongezeko la ajira kwa Watanzania Kwa asilimia 31 tofauti na mwaka 2022 kulikuwa na asilimia 20 pekee.
Alisema asilimia asilimia 98 ya Waajiliwa katika Mgodi huo ni Watanzania ambao asilimia 51 wanatokea Mkoa wa Mara mbali na hilo alisema Mgodi unafanya kuchangiaji kwa Serikali ambapo kuanzia 2019 hadi 2024 umechagia dora 3.97.
Aidha alisema wanafanya maendeleo mbali mbali ikiwemo shule ya msingi Kenyangi iliyojengwa katika Kata ya Matogo ,utunzaji wa mazingira kuhakikisha wanaongeza uelewa kuangalia maji ya sumu kuhakikisha hakuna madhara pamoja na kupambana na mararilia kuhakikisha Jamii inayozunguka Mgodi haipati Maria na 2024 wametenga bajeti ya bilioni 9 kutegeneza miradi 101 katika vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Kenyangi Khadija Sangi anashukuru Barrick Kwa ujenzi wa shule wa shule hiyo yenye vyumba vya madarasa 12 ambavyo vitapunguza adha ya msongamano wa wanafunzi darasani.
Alisema wanafunzi darasa la Saba wako 88 kwenye darasa moja kwenye shule hiyo wanayotakiwa kuhama na kuja kinyangi shule ya msingi ambapo Kwa taratibu za Serikali wanatakiwa wanafunzi 45 hivyo kupitia shule hiyo inayotarajia kufunguliwa rasmi January mkono mmoja utatakiwa kuwa na wanafunzi 45 au chini ya hapo.
Hata hivyo Mgodi huo unasimamia vikundi mbali mbali vya kilimo cha mboga mboga mafunzo ambayo yalianzishwa na Mgodi huo Kwa lengo la kuinua Jamii kiuchumi ikiwa ni moja ya njia bora ya kujiajiri kuliko kuamini kuwa ni lazima ivamie mabaki ya dhahabu