EMEDO na TMA waja mfumo mpya wa utoaji taarifa ya hali ya hewa kwa wavuvi

GEORGE MARATO TV
0

Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) na Mamlaka ya Utabiri wa hali ya hewa Mwanza wametambulisha mfumo mpya wa utoaji wa taarifa ya hali ya hewa kwa jamii ya wavuvi walioko katika kisiwa cha Goziba mkoani Mwanza.

Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 01/10/2024 katika kisiwa cha Goziba na kuhudhuliwa na Wavuvi,Wamiliki wa Mitumbwi,Wafanyabiashara wa Samaki na Vingozi wa Serikali.


Utafiti uliofanywa na Shirika la EMEDO mwaka 2021 ulibaini sababu mbalimbali zinazopelekea Wavuvi kuzama maji na wengine kupoteza maisha na sababu moja wapo ilibainika kuwa ni changamoto ya upatikanaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa wakati na uelewa kuhusu taarifa zenyewe na ili kutatua changamoto hiyo EMEDO na TMA wamefanikiwa kuja na mabango yatakayotoa taarifa za hali ya hewa kwa jamii ya wavuvi kwa njia rahisi na kwa kuanza wameanza na kisiwa cha Goziba.


Akizungumza katika uzinduzi rasimi wa mabango hayo Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa kanda ya ziwa Augustino Nduganda amesema nimuhimu kwa wadau wote wa uvuvi kupata taarifa sahihi za hali ya hewa kwaajili ya maisha yao na mali zao.


“Tumefikia hatua hii ndugu zangu kutokana na utafiti uliofanywa na wenzetu wa EMEDO hivyo tulikaa chini na tukajiuliza tuje na mfumo gani utakao kuwa rahisi kwenu tukapata jawabu la mfumo huu na bila shaka mnaona hata kwa picha tu unajua hali ya hewa leo ikoje”.alisema Nduganda

Meneja Nduganda amesema taarifa hii ya hali hewa itakuwa ikitolewa saa sita mchana kwaajili ya wachakataji wa mazao ya ziwa wajue hali ya hewa ilivyo na saa tisa alasiri kwaajili ya wavuvi wanaojiandaa kuingiwa ziwani.


Kwa upande wake meneja wa mradi wa kuzui kuzama maji kwa wavuvi kutoka EMEDO,Arthur Mugema ametoa wito kwa jamii ya wavuvi kutumia mabango hayo ya utabiri kabla ya kuingia ziwani kwa kuwa hicho ndicho kitu walichokuwa wakikitaka na kimefanyiwa kazi.

“Kupitia mradi huu wa kuzuia kuzama maji tumekuwa tukijitahidi kutatua changamoto moja baada ya nyingine tukiongozwa na utafiti tuliofanya mwaka 2021 mtakumbuka suala hili la kutopata taarifa sahihi za hali ya hewa nazo zilionekana kuwa tatizo”.alisema Mugema
 meneja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top