Rc Mtambi atuma salam za shukrani kwa Rais Dkt.Samia kwa kupokea fedha nyingi za miradi mara

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Butiama

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene kufikisha salam kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwaajili ya miradi.

Shukrani hizo amezitoa leo oktoba 3 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Nyamisisi baada ya kuzindua shule mpya ya msingi Chief Manyori.

Amesema mkoa wa Mara chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan umepokea kiasi cha tilioni 1 na zaidi ya bilioni 200 ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali.

Kanali Mtambi amesema 280 ikiwa ya shule,maji,afya,miundombinu na mingine ipo iliyokamilishwa na mingine inaendelea kutekelezwa.

" Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Mara tunaomba utufikishie salam kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mema sliyowanyia wananchi wa mkoa wa Mara.

" Miradi inaendelea vizuri na inasimamiwa vizuri na sio shule hii pekee ambayo umeizindua zipo shule mpya zaidi ya 10 hapa Butiama tunashukuru sana",amesema.

Akizungumza na wananchi wa Butiama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amesema atafikisha salam kwa Rais Dkt. Samia zilizotolewa na viongozi wa Butiama na mkoa wa Mara.

Amesema amelidhika na usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa na serikali kwaajili ya miradi mbalimbali ambayo amejionea tangu alipofika mkoa wa Mara.

Simbachawene amesema salam zilizotolewa kwenda kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na viongozi wakiwemo wa Chama cha Mapinduzi ( CCM)

 "Niwashukuru sana wananchi wa Butiama kwa mapokezi yenu na mkutano mzuri niwaahidi  kufikisha salam zenu zote mlizozitoa na pamoja na maombi kwa mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ikiwa leo ni siku ya 3 ya ziara yake mkoani Mara Waziri Simbachawene ametembelea wilaya za Serengeti na Butiama na kesho oktoba 4 atamalizia wilayani Bunda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top